Serikali yaahidi kujenga upya daraja hatari la Nithi lililoko Tharaka Nithi

“Pia tulijadili masuala yanayohusu Daraja la Nithi, ambalo limekuwa doa kwa sababu ya muundo wake mbovu.

Muhtasari
  • Akikutana na viongozi kutoka Kaunti ya Tharaka Nithi, wakiongozwa na Gavana Muthoni Njuki, katika afisi yake Nairobi
WAZIRI WA UCHUKUZI KIPCHUMBA MURKOMEN
Image: TWITTER

Waziri wa Uchukuzi, Kipchumba Murkmomen, Jumatatu, amesema kuwa serikali ilikuwa na nia ya kubuni upya daraja la Mto Nithi.

Akikutana na viongozi kutoka Kaunti ya Tharaka Nithi, wakiongozwa na Gavana Muthoni Njuki, katika afisi yake Nairobi, Waziri huyo aliangazia hatua nne ambazo zitachukuliwa.

“Pia tulijadili masuala yanayohusu Daraja la Nithi, ambalo limekuwa doa kwa sababu ya muundo wake mbovu.

"Tayari tumeanza mchakato wa kuzuia kupoteza maisha zaidi papo hapo," CS alibainisha.

Kulingana na Waziri  huyo, Rais Ruto, alitamani mabadiliko hayo yafanywe ndani ya muda mfupi, ili kupunguza kupoteza maisha zaidi.

Hatua hii ya kuzuia itapunguza idadi ya migongano ya ana kwa ana iliyorekodiwa kati ya magari.

Samani za barabarani kama alama za onyo zitawekwa ili kuwaongoza madereva na kuonyesha vikomo vya mwendo pia.

Daraja la Nithi ni mojawapo ya sehemu mbaya zaidi katika barabara kuu ya Nairobi-Meru, kurekodi ajali kadhaa, kutoka kwa migongano ya ana kwa ana  na magari kutumbukia mtoni.