KANU: Hatuwatambui wanachama waliohamia UDA

Nick Salata alifurushwa kama Katibu mkuu

Muhtasari

• Goerge Wainaina alisema kuwa KANU haitawachukulia kirahisi watu wanaojaribu kuchafua jina la chama.

Katibu mkuu wa Kanu Nick Salat.
Katibu mkuu wa Kanu Nick Salat.
Image: MAKTABA

Viongozi wa chama cha KANU sasa wamesema kwamba hawawatambui wanachama waliogura chama hicho na kuingia kwa chama cha UDA.

Viongozi hao walisema hilo baada ya baadhi ya viongozi wa KANU akiwemo Nick Salat kujiunga na chama cha UDA wakiwa wamevalia nguo za KANU kuashiria kuwa chama hicho kimejiunga na chama cha UDA.

Katibu mkuu wa KANU, George Wainanina ,alisema kuwa wanachama wa KANU waliobaki hawatagura kujiunga na chama chochote kama alivyofanya Nick Salat na wanachama wwengine.

Katibu mkuu huyo alisema kuwa wanaodai kuwa walikuwa wanachama wa KANU waliandikwa hivyo basi hawafai kutambulishwa kama wanachama wa chama hicho.

"Kinachotushtua ni matumizi  mabaya ya bidhaa za chama chenye thamani kubwa kuomba makombo ya mkate kutoka kwa serikali iliyojaa hadi ukingo  na wahusika waliokodishwa ," ilisoma sehemu ya taarifa hiyo.

Katibu mkuu Wainaina ailizidi kumnyooshea kidole Salat kwa kuendesha sarakasi, aikithibitisha kuwa  chama hicho hakitawachukulia kirahisi watu wanaojaribu kuchafua jina la chama.

Aliongeza kuwa chama hakijachanganyikiwa na hatua hiyo inayodaiwa . "Kile ambacho hatutasema uwongo ni watu binafsi kuhamaki kutoka mkutano mmoja hadi mwingine, kuwahadaa Wakenya chini ya uficho wa chama chetu tunachopenda," akabainisha.

"Tunataka kuwaambia kwamba KANU, iliyojengwa kwa msingi imara sana, haijaguswa na uasi wao unaodaiwa." Alisema kuwa KANU itasalia kujitolea kusalia imara na umoja katika kukuza demokrasia, umoja wa kitaifa na haki ya kijamii.

Siku ya Jumatano, Salat alidai kuwa ameongoza timu kutoka KANU hadi UDA, na kwamba wengine pia wana nia ya kuhama.