Kwa nini hakuna nafasi ya mazungumzo ya Ruto-Raila-Cherargei

"H.E Ruto ndiye anayesimamia nchi kikamilifu hakuna uhuni wala vitisho vitazuia urekebishaji

Muhtasari
  • Akizungumza siku ya Alhamisi, mbunge huyo alidai kuwa muungano wa Azimio la Umoja One ndio waanzilishi wa uvunjaji sheria.
Seneta wa Nandi Samson Cherargei
Image: EZEKIEL AMING'A

Seneta wa Nandi Samson Cherargei ameeleza ni kwa nini utawala wa Kenya Kwanza hautashiriki mazungumzo yoyote na upinzani.

Akizungumza siku ya Alhamisi, mbunge huyo alidai kuwa muungano wa Azimio la Umoja One ndio waanzilishi wa uvunjaji sheria.

"Hakuna nafasi ya mazungumzo kati ya Azimio-Oka na Rais William Ruto kwa sababu ni wabunifu wa wahujumu uchumi, machafuko na uvunjaji sheria," Cherargei alisema.

Seneta huyo wa UDA  amesisitiza kuwa Rais William Ruto hawezi kudhulumiwa.

Cherargei alisema hakuna chochote kutoka kwa muungano unaoongozwa na Raila Odinga kitakachomzuia Ruto kurekebisha nchi.

"H.E Ruto ndiye anayesimamia nchi kikamilifu hakuna uhuni wala vitisho vitazuia urekebishaji wa uchumi na mabadiliko," Cherargei alisema.

Aizungumzia maandamano yanayoendelea, seneta huyo alisema kuwa kinara wa upinzani Raila Odinga anafaa kubeba gharama ya uharibifu wowote wa mali ambapo matukio yatakuwa ya vurugu.

"Hasara ya mali au maisha kupitia Maandamano Tinga inapaswa kubeba gharama zote za uharibifu ikiwa maandamano hayatakuwa ya amani!" Cherargei alisema.