Raila ana mamilioni ya wafuasi wanaomwabudu-Alinur asema huku akimshauri Rais haya

"Rais William Ruto na Naibu wake Rigathi Gachagua wanapaswa kumtafuta Raila Odinga na kuzungumza kama waungwana.

Muhtasari
  • Matamshi ya Alinur yanajiri saa chache baada ya seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kusema kwamba Serikali ilikaidi wito wao wa mazungumzo.
ALINUR MOHAMED
Image: KWA HISANI

Mwanasiasa na mfuasi sugu wa Azimio Alinur Mohamed amemtaka rais William Ruto nanaibu wake Rigathi Gachagua kumtafuta waziri mkuu wa zamani Mhe Raila Odinga wafanye mazungumzo naye kabla mambo hayajaharibika.

Kulingana naye waziri mkuu wa zamani Mhe Raila Odinga bado ana mamilioni ya wafuasi wanaomwamini licha ya kushindwa katika uchaguzi wa urais wa 2022.

"Rais William Ruto na Naibu wake Rigathi Gachagua wanapaswa kumtafuta Raila Odinga na kuzungumza kama waungwana. Kenya ni kubwa kuliko sisi sote. Hatuwezi kufikiria hali ambapo Kenya inakuwa Sudan mpya. Raila ana mamilioni ya wafuasi wanaomwabudu, hatuwezi kupuuza hilo". Alisema Mhe. Alinur Mohamed.

Kumbuka kuwa rais William Ruto yuko kwenye rekodi akidai kuwa hatakubali hendisheki na aliyekuwa waziri mkuu Mh Raila Odinga kama serikali iliyopita.

Pia waziri huyo wa zamani alidai kwamba hataki hendisheki na mkuu wa nchi.

Matamshi ya Alinur yanajiri saa chache baada ya seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kusema kwamba Serikali ilikaidi wito wao wa mazungumzo.