Mwanamume ajitoa uhai baada ya kumuua kaka yake Mwingi

Baada ya tukio hilo, mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 32 alifariki kwa kujitoa uhai baada ya kujinyonga ndani ya nyumba yake.

Muhtasari
  • Mwendwa Katumani, jirani alisema wawili hao walikula kiamsha kinywa pamoja kisha baadaye kaka mdogo akaenda kulima shamba lao la familia.
Mwanamume ajitoa uhai baada ya kumuua kaka yake Mwingi
Image: LINAH MUSANGI

Mwanamume mwenye umri wa miaka 32 kutoka Muliluni huko Mwingi Magharibi alimdukua mdogo wake wa miaka 24 kwa kutumia panga akiwa kwenye shamba la familia yao.

Baada ya tukio hilo, mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 32 alifariki kwa kujitoa uhai baada ya kujinyonga ndani ya nyumba yake.

Mwendwa Katumani, jirani alisema wawili hao walikula kiamsha kinywa pamoja kisha baadaye kaka mdogo akaenda kulima shamba lao la familia.

"Kisha alimvamia akiwa shambani akitumia panga na kumwacha amelala ," alisema.

Alipelekwa katika Hospitali ya Mwingi Level 4.

"Baada ya kupata taarifa hizo, tulimtembelea hospitalini ambako alikuwa akishonwa nyuzi nyingi, alikuwa amekatwa sehemu ya nyuma ya kichwa, mikono na mgongo," Kitonga Muasya, jirani alisema.

Baada ya tukio hilo wanakijiji walianza kumfuatilia mhalifu huyo ambapo walivamia nyumba yake na kumkuta akining’inia kwenye paa la chumba chake kimoja

Hata hivyo, kijana huyo wa miaka 24 alifariki alipokuwa akipokea matibabu.

Akithibitisha kisa hicho, kaimu kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Mwingi ya Kati, Kazungu Charo alisema miili ya wawili hao imehamishiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Mwingi Level 4 huku uchunguzi ukianza.