logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Malala kushtaki Azimio kwa uharibifu wakati wa maandamano Jumatatu

Malala alidai kuwa maandamano iliyofanywa na Azimio ilileta uharibifu.

image
na

Habari22 March 2023 - 05:45

Muhtasari


•Malala alisema ataiomba mahakama kusitisha utoaji wa fedha za vyama vya siasa hadi suala hilo litakaposikizwa na kuamuliwa.

Aliyekuwa seneta wa Kakamega Cleophas Malala akimkejeli Raila kuwa amekuwa akihisi uchungu kupoteza mara 5

Katibu mkuu wa chama cha UDA, Cleophas Malala ameapa kushtaki muungano wa Azimio kwa kuandaa maandamano ya vurugu siku ya Jumatatu katika miji ya Nairobi na Kisumu.

Akizungumza katika mahojiano kwenye Citizen TV siku ya Jumanne, Malala alidai kuwa Odinga aliwalipa watu kuharibu ofisi  ya chama cha UDA iliyofunguliwa hivi majuzi katika jiji la Kisumu.

Malala alisema kuwa ataandika barua kwa msajili wa vyama vya kisiasa, Ann Nderitu na kumweleza wakili  wa chama hicho kushtaki chama cha ODM katika mahakama ya kuu ili kukishinikiza chama hicho kuajibikia uharibifu uliosababishwa siku ya Jumapili.

"Ni vibaya kuwa waandamanaji waliolipwa na ODM walienda kuchoma afisi zetu  za UDA,"

Aliongezea kuwa ataiomba mahakama kusitisha utoaji wa fedha za vyama vya kisiasa hadi suala hilo litakaposikizwa na kuamuliwa.

Malala alidai pia kuwa hatua ya UDA kuanzisha ofisi zake Kisumu haitasambaratishwa na maandamano ya Azimio huku akiwaambia wanachama wa UDA katika jiji la Kisumu kwamba watarudi kuzitengeneza ofisi hizo upya.

"Tunawaambia watu wetu wa Kisumu kwamba Jumanne tunarudi kupaka rangi upya , hiki ndicho chama tawala, si kama chama kingine tu.Tutaendelea na harakati za wanachama na Kisumu itakuwa manjano," alisema.

Malala alisema kuwa hawatashinikwa na Azimio kususia bidhaa za makampuni fulani kwani hata wao wanaweza kutoa wito wa kususia makampuni mengine.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved