Polisi lazima walinde Wananchi,la sivyo hasla watafanya hivyo-Cherargei

Alisema mamlaka lazima itumie mbinu zote zinazopatikana kutekeleza utaratibu dhidi ya 'mabwanyenye'.

Muhtasari
  • Akizungumza siku ya Jumatatu, seneta huyo alisema ikiwa polisi watashindwa kufanya hivyo, basi watalazimika kuingilia kati.
Seneta wa Nandi, Samson Cherargei
Seneta wa Nandi, Samson Cherargei
Image: Facebook//Cherargei

Seneta wa Nandi Samson Cherargei sasa anasema kwamba lazima polisi walinde maisha na mali ya Wakenya wote.

Akizungumza siku ya Jumatatu, seneta huyo alisema ikiwa polisi watashindwa kufanya hivyo, basi watalazimika kuingilia kati.

Alisema mamlaka lazima itumie mbinu zote zinazopatikana kutekeleza utaratibu dhidi ya 'mabwanyenye'.

"Leo ni siku ya kawaida ya kufanya kazi kote nchini. Polisi lazima walinde maisha na mali ya Wakenya wote wakishindwa kufanya hivyo hasla watajitokeza na kufanya hivyo. Polisi lazima watumie mbinu zote ikiwa ni pamoja na nguvu kurejesha akili na utawala wa sheria dhidi ya mabwanyenye wa Tinga/ wanarchists," alisema.

Matamshi ya Cherargei yanakuja kabla ya maandamano yaliyopangwa kufanywa na Upinzani unaoongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga.

Maandamano hayo yaliyoanza Jumatatu wiki jana yalishuhudia biashara zikiendelea kufungwa katika maeneo mengi ya jiji hilo, huku polisi wakiendesha vita na wafuasi wa upinzani.

Siku ya Ijumaa, Azimio alitangaza kuwa maandamano hayo yangeanza saa 6 asubuhi na kumalizika saa kumi na mbili jioni, Jumatatu na Alhamisi, kuanzia wiki hii.

Hata hivyo, kuanzia saa mbili asubuhi siku ya Jumatatu, maandamano yalikuwa bado kuanza.

Maduka mengi pia yanasalia kufungwa huku wafanyabiashara wakifuatilia kwa karibu hali hiyo.