logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Eric omondi amtoa jela mwendesha bodaboda aliyenaswa akilia mahakamani

Mashabiki walimsifia Eric kwa kitendo hicho cha ukarimu

image
na Radio Jambo

Yanayojiri13 April 2023 - 13:06

Muhtasari


  • Katika video hiyo mwendesha bodaboda huyo alilia  kwa uchungu huku akidai kuwa hana uwezo wa kulipa dhamana hiyo ambayo mahakama ilimtoza kwa kosa ambalo bado halijafahamika.

Mapema leo,mwendesha bodaboda alinaswa kwenye kanda ya video akilia bila kujizuia mahakamani baada ya hakimu kumzaba kwa dhamana elfu ishirini na tano.

Katika video hiyo mwendesha bodaboda huyo alilia  kwa uchungu huku akidai kuwa hana uwezo wa kulipa dhamana hiyo ambayo mahakama ilimtoza kwa kosa ambalo bado halijafahamika.

Eric Omondi alijibu upesi na kuelekea katika gereza la Industrial area ambapo alifanikiwa kumtoa jela mwendesha bodaboda huyo kwa  kulipa dhamana aliyokuwa amepewa.

Wanyonge ndio wanaumia,unaweza aje kumtoza mwendesha bodaboda dhamana ya elfu ishirini na tano, Leo tumemwachilia Fredrick kutoka Industrial Area Prison na tukamfanyia Shopping, Asante @spotonvacations kwa ununuzi.  KARIBUNI SANA MENGI YATABADILIKA!!!  WAKATI WETU UNAFIKA!!!!  Asante sana @gadaphylicha kwa kuja kupitia MUNGU IBARIKI BRO!!!"Alizungumza eric baada ya kumtoa mwendesha bodaboda huyo jela.

Mashabiki walimsifia Eric kwa kitendo hicho cha ukarimu na hizi hapa baadhi ya hisia za wanamitandao;

dela_gatta: This is touching...may God bless you eric

spotonvacations: Hebrews 13:16 Do not neglect to do good and to share what you have, for such sacrifices are pleasing to God.

lthebiggafiga: Gods Plan ❀️ love you for this keep pushing change will come power to the people

fatuomakeup: πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘ Good job Eric aki shida umaskini kukosa pesa ni mbaya sana kwa hii dunia😭

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved