logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Askofu mkuu Anthony Muheria ataka Serikali kukagua utajiri wa viongozi wote wa dini

Kulingana na Muheria, serikali inafaa kubuni sheria za kudhibiti dini potofu

image
na Radio Jambo

Habari26 April 2023 - 16:43

Muhtasari


  • Kulingana na Muheria, serikali inafaa kubuni sheria za kudhibiti dini potofu ili kuwang'oa viongozi ghushi ambao wana nia ya kuwapotosha wafuasi wao.
Askofu Anthony Muheria

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Nyeri Anthony Muheria sasa anawataka viongozi wote wa kidini kutangaza hadharani utajiri wao wa kifedha, kufuatia habari za mauaji ya watu wa kidini ya Shakahola ambayo yamewakera wengi baada ya takriban watu 90 kuripotiwa kufariki.

Akihutubia wanahabari siku ya Jumatano, Askofu Mkuu Muheria aliibua wasiwasi kuhusu kuibuka kwa viongozi wengi wa kiroho wanaodai kuwa walimu wa kidini wakati wanataka kuwalaghai watu wasiotarajia na walio hatarini.

Kwa hivyo, Muheria alitoa maoni kwamba serikali inapaswa kuingia na kukagua mapato ya viongozi wa kiroho ili kujenga uwajibikaji zaidi na kuepusha hali kama hizo.

“Ni muhimu tukague utajiri wa viongozi wote wa dini; sisi sote ikiwa ni pamoja na mimi mwenyewe tunapaswa kutangaza nilichonacho kwenye akaunti yangu,” alisema.

“Na inapaswa kuwa jambo la hadharani kwa Wakristo wote wanaofuata kanisa langu. Wanapaswa kujua ni kiasi gani ninacho na ninamiliki kiasi gani. Hiyo ndiyo njia pekee ya kutaniko liwezalo kulindwa kutokana na pupa ya viongozi wowote wa kidini wakorofi.”

Askofu Mkuu alizungumzia tukio la Shakahola, na kukanusha neno ‘uoshaji ubongo’ ambalo limekuwa sawa na hilo, badala yake alitaja mambo yanayoendelea hivi sasa kuwa ni vitendo vya ulaghai na ghiliba za makundi hatarishi katika jamii yanayofanywa na viongozi wa makanisa.

Kulingana na Muheria, serikali inafaa kubuni sheria za kudhibiti dini potofu ili kuwang'oa viongozi ghushi ambao wana nia ya kuwapotosha wafuasi wao.

"Tunasisitiza kwamba lazima kuwe na sheria za kudhibiti dini-ghushi, madhehebu na mikusanyiko...ni ubunifu wa kibinadamu wa mtu ambaye anataka kudanganya," alieleza.

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved