logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Macomrade' kupokea mikopo ya HELB moja kwa moja kupitia M-Pesa

Kwa muda mrefu, HELB wamekuwa wakitoa mikopo kwa wanafunzi kupitia akaunti za benki.

image
na Radio Jambo

Makala28 April 2023 - 10:26

Muhtasari


• Suluhisho la malipo ya pochi ya simu sasa linapatikana kupitia Safaricom M-PESA Mini App na HELB USSD *642#.

Wanafunzi vya elimu ya juu kupokea HELB kupitia M-Pesa.

Bodi ya mikopo ya elimu ya taasisi za juu HELB imetangaza kuwa imefanikiwa kupata ushirikoano na kampuni ya mawasiliano ya Safaricom ambapo itawawezesha kuanza mpango wa kutuma mikopo hiyo moja kwa moja kwa wanafunzi kupitia mfumo wa M-Pesa.

Afisa mkuu mtendaji wa bodi hiyo, Charles Ringera akizungumza mjini Mombasa ambapo wananchama wa bodi hiyo walikuwa na mkutano wa majadiliano kuhusu jinsi ya kuboresha huduma zao kwa wananfunzi wa vyuo vikuu na vyuo anuwai.

Ringera alisema sasa ni rasmi HELB itafunguliwa pochi kwenye mfumo wa M-Pesa ambapo kila mwanafunzi ambaye amejisajili kama mnufaishwaji wa mkopo huo atapokea hela hizo.

“Ni rasmi! HELB imeshirikiana na @Safaricom_Care MPesa kutoa mikopo ya wanafunzi kupitia pochi ya MPesa HELB,” ukurasa rasmi wa HELB ulitoa taarifa hiyo kupitia Twitter.

Suluhisho la malipo ya pochi ya simu sasa linapatikana kupitia Safaricom M-PESA Mini App na HELB USSD *642#.

"Suluhisho hilo linawawezesha wanufaika kutuma maombi ya mikopo inayofuata, kupata fedha za uhifadhi wa HELB, kutoa fedha, kuangalia hali ya mkopo, kupata taarifa za mkopo na kurejesha mikopo, yote kutoka kwa simu za kawaida, programu ya Android na iPhone," Ringera alisema.

Taarifa hizi zinakuja kipindi ambapo wengi wa wanafunzi wanufaikaji wa mikopo hiyo wamekuwa wakilalama kuhusu kucheleweshwa kwa mikopo hiyo hali ambayo imefanya maisha yao vyuoni kuwa magumu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved