logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kanini Kega afutilia mbali mkutano uliopangwa na Uhuru

Kanini Kega amefutilia mbali mkutano wa wajumbe ulioitishwa na Rais msataafu Uhuru.

image
na Radio Jambo

Habari10 May 2023 - 05:56

Muhtasari


• Mbunge wa EALA Kanini Kega amefutilia mbali kongamano la wa wajumbe wa wa Jubilee lililoitishwa na Rais msataafu Uhuru Kenyatta.

• Katika taarifa iliyotiwa saini na Kanini Kega mrengo wake ulinasema chama hicho kitatoa notisi ya kuitisha kongamano maalum la Wajumbe wa Kitaifa.

Mbunge wa bunge la Afrika mashariki Kanini Kega na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta

Mbunge wa bunge la Bunge la Afrika Mashariki Kanini Kega amefutilia mbali kongamano maalum la wajumbe wa kitaifa lililoitishwa na kiongozi wa chama cha Jubilee Rais msataafu Uhuru Kenyatta.

Mzozo katika choma hicho umeongezeka baada ya upande unaoongozwa na Kega na ule  wa Jeremiah Kioni kuendelea kuzozana kuhusu uongozi wa chama hicho.

Katika taarifa iliyotiwa saini na Kega kundi hilo linasema chama hicho kitatoa notisi ya kuitisha kongamano maalum la Wajumbe wa Kitaifa.

“Fahamu kuwa kamati kuu ya kitaifa ya chama cha Jubilee (NEC) imefutilia mbali notisi ya kongamano maalum la wajumbe wa kitaifa iliyochapishwa kwenye vyombo vya habari tarehe 29, Aprili” ilisoma sehemu ya taaarifa hio ya Kanini Kega.

Tarehe 29 mwezi wa Aprili, Kenyatta aliitisha mkutano maalum ambao alisema utafanyika tarehe 22,Mei.

Katika notisi iliyotiwa Saini na Rais mstaafu Kenyatta, chama hicho kilisema ajenda ya kongomano hilo ni kukagua, kuunda na kuidhinisha sera za chama Pamoja na kupokea taarifa ya hali ya chama kutoka kwa kamati kuu ya kitaifa na kuzingatia na kuidhinisha mambo mengine yote.

Wiki iliyopita mrengo wa Kega ulitangaza kumtimua Uhuru kama kiongozi wa chama cha jubilee huku mizozo katika chama tawala cha zamani ukizidi.

Mrengo wa Kega ilitamtangaza mbunge maalum Sabina Chege kuwa kaimu kinara wa chama  katika mkutano uliyofanyika tarehe 2, Mei 2023.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved