Chama cha wamiliki wa matatu nchini kuongeza nauli kuendana na bei mpya ya mafuta

Ongezeko hili linamaanisha bei ya petroli imeongezeka hadi shilingi 182.70, ile ya dizeli ikipanda hadi 168.40 na mafuta taa yatauzwa kwa shilingi 161.13 jijini Nairobi.

Muhtasari
  • Mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa matatu (daladala) nchini , Samuel Kimutai akizungumza amesema kuwa serikali inapaswa kurejesha ruzuku.

Chama cha wamiliki wa matatu nchini Kenya wamesema hawana budi bali kuwatwisha abiria mzigo huo wa bei ya mafuta kwa kuongeza nauli kuendana na bei mpya ya mafuta ya petroli na dizeli.

Mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa matatu (daladala) nchini , Samuel Kimutai akizungumza amesema kuwa serikali inapaswa kurejesha ruzuku.

"Serikali inafaa kufikiria kurejesha ruzuku hizo kwani hii inaathiri Wakenya wanaoenda kwenye shughuli zao za kila siku ili kukuza uchumi," alisema Kimutai.

Jumapili, Mei 14, EPRA iliongeza bei za Super Petrol, Dizeli na Mafuta ya Taa kwa Ksh3.40 kwa lita, Ksh6.40 kwa lita na Ksh15.19 kwa lita mtawalia.

Ongezeko hili linamaanisha bei ya petroli imeongezeka hadi shilingi 182.70, ile ya dizeli ikipanda hadi 168.40 na mafuta taa yatauzwa kwa shilingi 161.13 jijini Nairobi.

“Kwa mujibu wa Kifungu cha 101(y) cha Sheria ya Petroli ya 2019 na Notisi ya Kisheria Na.192 ya 2022,EPRA imepania kubadilisha bei za juu zaidi za rejareja na za jumla za bidhaa za petroli ambazo zitaanza kutumika kuanzia tarehe 15Mei hadi tarehe 14 Juni 2023.” Taarifa hio ilisoma.