Washukiwa 3 wakamatwa kufuatia kutoweka kwa mtoto Nairobi

Siku iliyofuata, mtoto huyo alikabidhiwa kwa mshukiwa wa pili ambaye pia anashukiwa kumnajisi.

Muhtasari
  • Polisi Jumatatu walisema washukiwa watatu wako kizuizini kufuatia kutoweka kwa msichana wa miaka 14 mnamo Mei 9, katika kituo cha reli cha Nairobi.
Pingu
Image: Radio Jambo

Wanaume wawili na mwanamke mmoja wamekamatwa kama washukiwa wa kesi ya kutoweka kwa mtoto wa miaka 14.

Polisi Jumatatu walisema washukiwa watatu wako kizuizini kufuatia kutoweka kwa msichana wa miaka 14 mnamo Mei 9, katika kituo cha reli cha Nairobi.

"Kulingana na babake mtoto, bintiye alikuwa akisafiri kutoka Mombasa kwenda Nairobi kwa treni ya saa tisa jioni alipotoweka alipofika Nairobi baadaye usiku huo," DCI iliandika kwenye Twitter.

Polisi walisema bila kujulikana kwa baba aliyefadhaika, mtoto huyo alifika kwenye kituo cha Nairobi mjini mwendo wa saa tatu unusu usiku na kutoroka nje ya kituo hicho akiwa na mwanamume baadaye.

Polisi walisema kuwa simu za baba aliyekuwa na wasiwasi kwa simu ya bintiye hazikupokelewa huku akitoweka na mwanamume huyo hadi Riruta Satellite huko Dagoretti, ambako inadaiwa alinajisiwa.

Siku iliyofuata, mtoto huyo alikabidhiwa kwa mshukiwa wa pili ambaye pia anashukiwa kumnajisi.

Mshukiwa wa tatu ni mwanamke aliyetambuliwa ambaye anadaiwa kusaidia kumhifadhi mtoto huyo.

"Washukiwa watatu wanaume wawili na mwanamke wako kizuizini kufuatia kutoweka kwa msichana wa miaka 14 mnamo Mei 9, 2023, katika kituo cha reli cha Nairobi.

"Jumla ya washukiwa watatu kufikia sasa wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo, akiwemo mwanamke anayeaminika kusaidia kumhifadhi mtoto huyo," DCI aliongeza.