Miguna ataka waliohusika katika kashfa ya Kemsa wakamatwe

Miguna alisema hii ndiyo njia pekee ya kumaliza wizi uliopangwa katika afisi za umma.

Muhtasari
  • Ujumbe wake unajiri baada ya Rais William Ruto kumfukuza kazi Waziri wa Afya na bodi nzima ya Mamlaka ya Ugavi wa Dawa nchini.
Jenerali Miguna hatimaye ametua nchini
Jenerali Miguna hatimaye ametua nchini
Image: Andrew Kasuku

Maafisa wa serikali waliouza sukari iliyopigwa marufuku kwa matumizi ya umma wanapaswa kukamatwa na kushtakiwa, haya ni maneno ya wakili Miguna Miguna aliyoyasema siku ya Ijumaa,kuhusina na sakata ya Kemsa.

Miguna pia alisema yeyote aliyeiba au kujaribu kuiba pesa hizo Kemsa anafaa kukamatwa na kushtakiwa kwa uhalifu huo.

"Wanapaswa kukamatwa na kufunguliwa mashtaka na pesa za umma walizoiba au mapato waliyopata yarejeshwe kwa umma bila riba," alisema kwenye ukurasa wake wa twitter siku ya Ijumaa.

"Hawapaswi kulipwa nusu mshahara wala kuwa na nafasi ya kurejeshwa."

Miguna alisema hii ndiyo njia pekee ya kumaliza wizi uliopangwa katika afisi za umma.

Ujumbe wake unajiri baada ya Rais William Ruto kumfukuza kazi Waziri wa Afya na bodi nzima ya Mamlaka ya Ugavi wa Dawa nchini.

Haya pia yanajiri kufuatia hatua ya Rais kuwachambua maafisa 27 kuhusu kuachiliwa kwa sukari iliyopigwa marufuku kwa umma ambayo ilikuwa imetangazwa kuwa haifai kwa matumizi ya binadamu mnamo 2018.

Sukari hiyo, ambayo inasemekana kuwa na chembechembe za shaba, ilifika katika Bandari ya Mombasa mwaka wa 2018 lakini ikashutumiwa na Shirika la Viwango la Kenya kuwa ina madhara kwa matumizi ya binadamu.

Waziri wa Afya Susan Nakhumicha kwa upande wake aliunda upya bodi ya Kemsa na kuteua wanachama wapya.

Wanachama hao wapya ni pamoja na Hezborn Oyieko Omollo, Bernard Kipkirui Better, Jane Masiga na Jane Nyagaturi Mbatia.

Nakhumicha wakati pia amempiga kalamu afisa mkuu mtendaji wa KEMSA Terry Ramadhani na kumteua Andrew Mutava Mulwa kama kaimu Mkurugenzi.

Akizungumza wakati wa kikao na wanahabari Ikulu siku ya Jumapili, Ruto bila kufichua maelezo zaidi alisema ameanza kuangalia matatizo ya Kemsa.

"Ninafanya jambo kuhusu hilo. Utaona matokeo. Ninataka kukupa ahadi yangu, nitasafisha KEMSA, chochote kinachohitajika, chochote kinachogharimu," alisema.

Kemsa imeendelea kuteka vichwa vya habari kuhusu ufisadi na usimamizi mbovu.

Sakata ya kwanza ilikuwa takriban Sh7 bilioni zilizokusudiwa kununua vifaa vya kinga ya kibinafsi (PPE) na muhimu vya afya katika kilele cha janga la Covid-19 na kuishia kwenye mifuko ya watu wachache waliounganishwa vizuri.