Nesi maarufu kutoka Kitale, Lukresia Robai atumbuiza katika hafla ya WHO Geneva

Nesi maarufu aliyeonekana katika video zilizoenea mitandanoni akimtumbuiza mtoto mgonjwa katika hospitali ya Kitale awatumbuiza wageni katika kongamano la WHO mji wa Geneva

Muhtasari

β€’ Robai alikuwa miongoni mwa wateule waliowakilisha Afrika Mashariki katika sherehe za ufunguzi wa hafla hiyo.

β€’ Katika video iliyochapishwa na mwanahabari wa BBC Mercy Juma nesi huyo alionekana akisakata densi huku umati ukishangilia kwa vifijo.

George Natembeya na Elizabeth

Elizabeth Robai, Nesi maarufu aliyeonekana katika video zilizoenea mitandanoni akimtumbuiza mtoto mgonjwa katika hospitali ya Kitale awatumbuiza wageni katika kongamano la WHO mji wa Geneva, Switzerland.

Muuguzi huyo alikuwa akiwakilisha Shirika la Afya Duniani (WHO) wakati wa kikao cha 76 cha Baraza la Afya Duniani mjini Geneva.

Robai alikuwa miongoni mwa wateule waliowakilisha Afrika Mashariki katika sherehe za ufunguzi wa hafla hiyo.

Muuguzi huyo alipata umaarufu Novemba 2022, aliponaswa kwenye video akicheza dansi kwa mtoto akiyekuwa akiugua katika hopitali ya Rufaa ya Kitale.

Akiwa Geneva, aliwafurahisha wahudumu alipopiga dansi kwa wimbo maarufu wa Kiswahili β€˜Nimeuona Mkono wa Bwana.’

Katika video iliyochapishwa na mwanahabari wa BBC Mercy Juma nesi huyo alionekana akisakata densi huku umati ukishangilia kwa vifijo.

 

Mercy Juma alimsherehekea Elizabeth kwa densi yake ya kufana.

"Tumeuona, baba!" Wakati kanisa la East Africa na club banger likishiriki katika sherehe za ufunguzi wa #walkthetalk @WHO huko Geneva. Kuwa na uhakika, tuliwakilisha nchi ya mama vizuri. Vaibuuu! πŸ˜† 🀣 πŸ˜‚." Aliandika Mercy

 

Mnamo 2022 Robai alifichua kwamba alikuwa akizunguka katika wadi za hospitali alipomwona mvulana mgonjwa akiwa amevunjika mguu katika hali ya huzuni na akamua kumfurahisha mvulana kwa kudensi.

Video hiyo iliyochapishwa kwa mtandao wa  TikTok, ilipata maoni zaidi ya milioni moja ndani ya siku mbili pekee.

Baada ya video hio kuenea, Serikali ya Kaunti ya Trans Nzoia ilijitolea kumlipia karo ya shule na kumuahidi kazi baada ya kuhitimu kutoka chou cha mafunzo cha KMTC.

Mkutano huo wa Sabini na Sita wa shirika la afya Duniani(WHO) ambao unafanyika Geneva unakusudiwa kusherehekea miaka 75 ya shirika hilo kwa mada ya; kuokoa maisha, na afya kwa wote.