Polisi wawakamata washukiwa 3 kwa wizi wa Milioni 8 katika kituo cha mafuta

Washukiwa hao wanakabiliwa na kesi ya wizi kinyume na kifungu cha 281 cha kanuni ya adhabu

Muhtasari

• Washukiwa hao wanadaiwa kuingia ndani ya jengo hilo kupitia paa kabla ya kuziiba pesa hizo baada ya kuvunja sefu.

• Washukiwa hao waliotambulika kama David Mushendu, Moses Cherish na Eliud Wangai walipatikana na kima cha shinlingi milioni 2.5.

Kituo cha pampu ambapo pesa hiizo zinadaiwa kuibwa.
Kituo cha pampu ambapo pesa hiizo zinadaiwa kuibwa.
Image: DCI /FACEBOOK

Polisi wamewakamata washukiwa 3 kuhusiana na kutoweka kwa milioni 8 zilizoibwa kutoka kwa mfanyabiashara wa Kiambu.

Katika taarifa ya idara ya upelelezi na makosa ya jinai (DCI) kwenye akaunti yake ya Facebook polisi walisema pesa hizo zilizokuwa zimetoweka mwezi mmoja uliopita, ziliibiwa katika kituo cha mafuta ya petroli huko Kinangop, Nyandarua.

Washukiwa hao wanadaiwa kuingia ndani ya jengo hilo kupitia paa kabla ya kuziiba pesa hizo baada ya kuvunja sefu.

“Katika kisa hicho kilichoripotiwa mwishoni mwa mwezi uliopita na mke wa mfanyabiashara huyo, pesa hizo ziliibwa kwenye sefu iliyofichwa katika kituo cha mafuta kilichotelekezwa kilicho Kinangop, Nyandarua,” sehemu ya taarifa hio ilisoma.

Washukiwa hao waliotambulika kama David Mushendu, Moses Cherish na Eliud Wangai walipatikana na kima cha shinlingi milioni 2.5.

“Jumla ya Sh2.5 milioni zimepatikana kutoka kwa washukiwa,” taarifa hiyo ilisoma.

Washukiwa hao wanakabiliwa na kesi ya wizi kinyume na kifungu cha 281 cha kanuni ya adhabu.