SAHIHI YA MWUUNGANO

Sakaja atia mkataba wa maendeleo na Afrika Kusini

Kusini na Mashariki zimeunga kuendeleza utendakazi

Muhtasari

•Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja ametia sahihi  mkataba wa maendeleo na Hill-Lewis ambaye ni meya wa Cape Town  Afrika Kusini Jumanne 23.

•Sakaja, ambaye kauli yake wakati wa kampeni ilikuwa  “wacha tufaifanye  Nairobi ifanye kazi”,amekuwa akiendeleza kauli hiyo hasa kwa  baraza la kata hiyo kwa kuwapa magari mapya ndipo kufanikisha maendeleo.

Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja ametia sahihi  mkataba wa maendeleo na Hill-Lewis  meya wa mji wa Cape Town  Afrika Kusini.

Sakaja, ambaye kauli yake wakati wa kampeni ilikuwa  “wacha tufaifanye  Nairobi ifanye kazi”,amekuwa akiendeleza kauli hiyo hasa kwa  baraza la Kaunti hiyo kwa kuwapa magari mapya ndipo kufanikisha maendeleo.

 Katika mitandao yake ya kijamii alisema kuwa ,“Nina furaha kwa kuusaini mji dada wa Cape Town  kwa makubaliano na utawala wa meya  Hill-Lewis hivi leo. Nairobi na Cape Town ni majimbo makubwa katika bara letu.”

Sakaja  aliendelea na kusema kuwa, kusini na mashiriki mwa Afrika zimeungana pamoja ndipo kuendeleza utendakazi.Haya yanajiri huku baadhi ya vikwazo vilivyoyakumba mataifa haya mawili kuondolewa, ambapo gavana huyo alitaja kama nafasi  nzuri kwa watu katika mataifa yote mawili.

“Ushirikiano huu tumeafikiana kuondolewa kwa baadhi ya visa kati ya nchi hizi mbili na ambayo ni nafasi kubwa kwa watu.” Sakaja alisema.