Washukiwa wawili wakamatwa kwa madai ya kuiba Sh8 milioni

Watuhumiwa hao wawili wanakabiliwa na mashtaka ya wizi kinyume na kifungu cha 281 cha sheria ya kanuni ya adhabu.

Muhtasari
  • Ksh. Milioni 2.5 zimepatikana kutoka kwa washukiwa hao wawili huku msako mkali wa kumsaka mshukiwa wa tatu David Mushendu ambaye bado hajakamatwa.
Washukiwa wawili wakamatwa kwa madai ya kuiba Sh8 milioni
Image: DCI/TWITTER

Washukiwa wawili wamekamatwa kwa madai ya kuiba Ksh.8 milioni kutoka kwa mfanyabiashara wa Kiambu.

Kulingana na taarifa ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) pesa hizo ziliibwa kutoka kwa sefu iliyokuwa imefichwa katika kituo cha pampu kilichotelekezwa eneo la Kinangop, Kaunti ya Nyandarau.

Kesi hiyo iliripotiwa mwishoni mwa mwezi uliopita na mke wa mfanyabiashara huyo.

"Katika tukio lililoripotiwa mwishoni mwa mwezi uliopita na mke wa mfanyabiashara huyo, pesa hizo ziliibiwa kwenye sefu," ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.

DCI ilibaini kuwa washukiwa hao wawili, Moses Cherish na Eliud Wangai, waliingia kwenye jengo hilo kupitia paa na kuiba pesa hizo.

"Washukiwa hao wanaaminika kuwa waliingia ndani ya jengo hilo kupitia paa kabla ya kujisaidia na pesa hizo baada ya kuvunja sefu," DCI iliripoti.

Ksh. Milioni 2.5 zimepatikana kutoka kwa washukiwa hao wawili huku msako mkali wa kumsaka mshukiwa wa tatu David Mushendu ambaye bado hajakamatwa.

Watuhumiwa hao wawili wanakabiliwa na mashtaka ya wizi kinyume na kifungu cha 281 cha sheria ya kanuni ya adhabu.