Museveni atishia kuwatimua Wakenya kwa ajili ya wizi wa mifugo

Museveni alisema Wakenya wanaoishi Turkana watafukuzwa kwa kusafirisha bunduki haramu.

Muhtasari
  • Mwezi Aprili, mahakama ya Uganda iliwahukumu Wakenya 32 kifungo cha miaka 20 kila mmoja kwa kumiliki bunduki kinyume cha sheria.
Image: BBC

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametishia kuwatimua wakenya kutoka nchini mwake kutokana na wizi wa mifugo.

Katika agizo kuu la Mei 19, 2023, Museveni alisema Wakenya wanaoishi Turkana watafukuzwa kwa kusafirisha bunduki haramu.

“Ninawapa wakazi wa Turkana miezi sita kutekeleza maagizo yangu. Iwapo suala la bunduki kuingia Uganda kinyume cha sheria, kukabidhiwa kwa wahalifu walioua Wanajiolojia wetu au matumizi ya haki za kimila na kurudisha ng’ombe walioibiwa halitapatiwa ufumbuzi, sitakuwa na mbadala zaidi ya kuwafukuza wote. Turkana," alisema.

"... Hawataruhusiwa tena kuingia Uganda na ng'ombe wao."

"Hapa tahadhari inapaswa kutekelezwa kwa sababu watu wetu wanaweza kuwa wanatia chumvi idadi. Ili kurahisisha kazi ya utambuzi wa ng'ombe, serikali hizo mbili zinafaa kuratibu upigaji chapa wa ng'ombe ili kuonyesha wilaya na kaunti ndogo ya idadi ya ng'ombe," aliongeza.

Mwezi Aprili, mahakama ya Uganda iliwahukumu Wakenya 32 kifungo cha miaka 20 kila mmoja kwa kumiliki bunduki kinyume cha sheria.

Wafugaji hao wa Turkana walipatikana na hatia baada ya kukiri hatia.