Polisi wamelazimika kutumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wamekusanyika katika makao ya DCI yaliyopo barabara ya Kiambu Alhamisi 25.
Watu hao wanaoaminiwa kuwa wafuasi wa Maina Njenga,walivamia makao hayo ya idara ya upelelezi ili kudai kuachiliwa kwa kiongozi wao ambaye bado alikuwa amezuiliwa akihojiwa.
Njenga mwenyewe alijiwasilisha kwa maafisa wa polisi mjini Nakuru mnamo Mei 24, kuhojiwa.
Kiongozi huyo wa awali wa kundi la Mungiki amekuwa akizuiliwa katika makao hayo ya idara ya upelelezi huku akihojiwa kuhusiana na madai ya kupatikana kwa bunduki mbili pamoja na misokoto 90 ya bangi iliyopatikana katika makao yanayohusishwa naye eneo la Ngomongo kata ya Bahati.