MAUAJI YA SHAKAHOLA

Tutaokoa kila mtu kutoka Shakahola - Kindiki

Mackenzi analima kila aina ya chakula lakini wafuasi wake hufa njaa

Muhtasari

•Waziri wa usalama wa taifa na masuala ya ndani Prof. Kithure Kindiki  Alhamisi 25 alitua katika mji wa Malindi kaunti ya Kilifi kuongoza awamu nyingine ya upasuaji wa miili iliyofukuliwa katika msitu wa Shakahola.

•Haya yanajiri huku mtu mmoja aliyeokolewa katika msitu huo akifariki akiwa katika hospitali kwa kujinyima chakula.

Waziri wa usalama wa ndani  Kithure Kindiki  Alhamisi alitua katika mji wa Malindi kaunti ya Kilifi kuongoza awamu nyingine ya upasuaji wa miili iliyofukuliwa katika msitu wa Shakahola.

Haya yanajiri huku mtu mmoja aliyeokolewa katika msitu huo akifariki akiwa katika hospitali kwa kujinyima chakula.

Kwa wakaazi wa eneo la Malindi Kindiki alisema kuwa juhudi za kuwatafuta na kuwaokoa watu kutoka msitu wa Shakahola zinangali zinaendelea bila kutatizika.

Waziri huyo wa usalama aliendelea kusema kwamba,serikali itatengeneza barabara za usalama katika eneo la Chakama Ranch ili kuwezesha maafisa wa usalama pamoja na washikadau  wengine wanaolenga kuwaokoa watu kutoka msitu huo ndipo kupenya humo na kumwokoa mtu yeyote yule.

Kindiki kwa kuongeza alisema kuwa,alitembelea msitu wa Shakahola katika makaazi ya mhubiri Mackenzie na kuyaona maendeleo yake licha ya wafuasi wake kuangamia na kufa njaa. “Nimetembelea msitu wa Shakahola ambapo ndipo makao ya Mhubiri Mackenzie, ametengeneza mabwaga ya  maji,anaendesha ukulima wa vyakula vya kila aina licha ya kuwapa wafuasi wake itikadi kali za kukaa njaa hadi wafe.

Kindiki amesitisha shughuli za ufukuzi wa miili huku shughuli ya upasuaji wa maiti ikishika awamu ya pili.