logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanaume akamatwa baada ya kumuua msichana kikatili hadharani

Polisi wamewahusisha kimapenzi wanandoa hao na kusema walizozana saa kadhaa

image
na Radio Jambo

Makala29 May 2023 - 16:33

Muhtasari


  • Video hiyo, ambayo imesambaa mitandaoni na kusababisha hasira nchini India, inaonyesha watu wengi wakitazama shambulio hilo au wakitembea.

Polisi katika mji mkuu wa India, Delhi, wamemkamata kijana mwenye umri wa miaka 20 kwa kumdunga kisu kikatili na kumuua rafiki wa kike mwenye umri wa miaka 16 hadharani.

Picha za shambulio hilo zinaonyesha mwanamume huyo akimdunga kisu msichana mara kadhaa na kumponda kichwa kwa jiwe kubwa.

Video hiyo, ambayo imesambaa mitandaoni na kusababisha hasira nchini India, inaonyesha watu wengi wakitazama shambulio hilo au wakitembea.

Polisi wamewahusisha kimapenzi wanandoa hao na kusema walizozana saa kadhaa kabla ya mauaji siku ya Jumapili.

Msichana huyo alikuwa anaenda kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa kwa mtoto wa rafiki yake aliposhambuliwa, afisa mkuu wa polisi Ravi Kumar Singh aliambia shirika la habari la ANI.

Alimtaja mshukiwa kuwa ni Sahil na akasema alikamatwa kutoka karibu na wilaya ya Bulandshahr katika jimbo jirani la Uttar Pradesh.

Bw Singh aliongeza kuwa uchunguzi unaendelea na kwamba polisi hawakuweza kufichua maelezo zaidi kwa sasa.

Baada ya kusambaa kwa video za mauaji hayo ya kutisha, wengi walijitokeza kwenye mitandao ya kijamii kueleza hasira na ghadhabu.

Hashtagi kama vile mauaji ya Delhi na uhalifu wa Delhi zilikuwa zikivuma kwenye Twitter pamoja na Shahbad Dairy, jina la eneo ambalo uhalifu ulitokea.

Katika ujumbe wa Twitter , Waziri Mkuu wa Delhi Arvind Kejriwal alielezea mauaji hayo kama "ya kusikitisha sana" na akasema kwamba "wahalifu wamekuwa hawaogopi, hakuna hofu ya polisi".

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved