Sakaja aahidi kujenga daraja ya Njiru baada ya malalamishi mtandoni

Sakaja alitangaza mpango huo baada ya kushinikizwa na wakazi wa Nairobi mitandaoni.

Muhtasari

• Sakaja ameahidi kuwajengea daraja jipya wakazi wa wodi ya Njiru baada ya video iliyoangazia daraja hatari katika eneo hilo kusambaa mitandaoni.

• Sakaja aliongeza kuwa waandisi waliukuwa wanaunda mpango wa kutengeneza daraja mbadala ambalo litakuwa likitumika kihalali.

Gavana Johnson Sakaja.
Gavana Johnson Sakaja.
Image: TWITTER

Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja ameahidi kuwajengea daraja jipya wakazi wa wodi ya Njiru baada ya video iliyoangazia daraja hatari katika eneo hilo kusambaa mitandaoni.

Sakaja Katika akaunti yake ya Twitter aliwahikikishia wakazi wa eno hilo kwamba atawajengea daraja baada ya video ya mwanaume mmoja akivuka daraja hatari akilalamika kuhusu hali ya daraja hilo na kumsihi gavana huyo kuiangazia.

“Ukiangalia hapo chini hizi ni nyumba, hapa mtu akieza anguka hawezi baki, ile ni siweji ikielekea kwa mto, hii daraja liwekwe pahali pa kushikilia kwa kuwa watoto hupita hapa na wakieza anguka wataaga kwa hakika,”alisema mwanaume huyo.

Sakaja alimkosoa na kusema kuwa hilo halikukuwa daraja ila ni bomba la maji taka ambalo lilikuwa likitumika kama daraja.

“Hilo ni boma la maji taka la zamani ambalo limetumiwa kwa miongo kadhaa na wakaazi kuvuka. Haipaswi kutumika kama daraja,” alisema Sakaja.

Aliongeza kuwa wahandisi walikuwa wanabuni mpango wa kutengeneza daraja mbadala ambalo litakuwa likitumika kihalali.

Sakaja alisema maji hayo ya taka yaliyokuwa yakitiririka ni matokeo ya kilimo haramu ambapo aliwalaumu wakulima kelekeza maji hayo ya taka kwa mashamba yao.