Ulimwengu ulipoadhimisha Siku ya Akina Baba Jumapili, Juni 18, Mke wa Rais Rachel Ruto alisherehekea siku hiyo kwa kumthamini mwenzi wake, Rais William Ruto kwa kuwa baba anayewajibika na mwalimu mwema kwa watoto wao.
Katika ujumbe aliotuma kwenye akaunti yake ya Twitter, Mama wa Taifa alifananisha mtindo wa Ruto wa kuwajengea watoto maadili na babake mzazi.
“Nina kumbukumbu nyingi zenye kupendeza za baba yangu. Lakini kile ambacho kimekaa nami kwa miaka mingi ni nyakati zinazotumika kung'arisha viatu vyake. Baba yangu angenifanya ning'arishe viatu vyake mbele ya kioo. Na, wakati wowote nilipofikiri kuwa nimepata mng'ao kamili, angenifanya nipige mswaki zaidi. Mikono yangu michanga ingechoka hadi nipate kung'aa kabisa,” alisema.
Mkewe Rais alisema mumewe, ambaye alimtaja kwa jinala utani la 'Bill' amekuwa akiwaelekeza watoto wao kwa njia ifaayo, na kuwasihi wajitahidi kwa wanachofanya.
“Labda ni mambo ya kila baba. Kufundisha bila kusema. Leo, tunapoadhimisha Siku hii ya Akina Baba, ninasherehekea akina baba wote wanaowafundisha watoto wao kwamba, katika kila kitu wanachofanya, lazima wajitahidi "kufanya uangaze sawasawa!", aliongeza.
Rais na mkewen walifunga ndoa mwaka wa 1991.