Baraza linalosimamia vyombo vya habari (MCK) limeeleza hofu kuwa uhuru wa wanahabari upo hatarini baada ya waziri wa uekezaji, viwanda na biashara Moses Kuria kushambulia shirika la habari la Nation Media Group.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, baraza hilo lilisema kuwa matamshi ya waziri huyo katika ujumbe aliyoandika kwenyeTwitter ni tukio mbaya zaidi kuwahi kushudiwa tangu taifa lipate uhuru na inaidhalalaisha heshima ya nchi.
Waziri huyo siku ya Jumapili alitishia idara za serikali na kuzionya dhidi ya kufanya matangazo ya serikali katika kituo cha Nation huku akionya kuwa mtu atakayekiuka amri hiyo atapoteza kazi yake serikalini.
MCK katika taarifa yake ilikosoa amri ya mwaniuaji huyo wa zamani wa kiti cha ugavana katika uchaguzi mkuu uliopita ikisema kuwa hatua hiyo ni kinyume na katiba ya Kenya.
“Mwenendo huo wa waziri huyo inakiuka sura ya sita ya katiba ya Kenya kwa watumishi wa umma na uhuru wa wanahabari”
Baraza hilo lilisema kuwa kazi ya wanahabari ya kuiwajibisha serikali inafaa kupongezwa na kuongeza kuwa kazi hii mara nyingi huchukuliwa kama mashambulizi na kuwafanya watu fulani kuwa na wasiwasi.
Baraza hilo pia liliongeza kuwa limeitisha kikao cha dharura baina ya serikali na washikadau katika vyombo vya habari ili kuhakikisha uhuru wa wanahabari.
“Baraza la vyombo vya habari inafanya mazungumzo ya dharara na serikali na washikadau katika sekta ya habari kuzungumzia mahusiano baina ya serikali na vyombo vya habari ili kulinda uhuru wa wanahabari na kuhakikisha taarifa zinazowahusu umma zinaripotiwa kwa umakini.”
Baraza hilo pia lilisema kuwa mazungumzo hayo yanatarajia kuweka njia mwafaka ya kusuluhisha migogoro itakayo ibuka baina ya seikali na vyombo vya habari.
Baraza hilo la wanahabari imevunja kimya kutokana na kile ilionekana ni makabilioano ya moja kwa moja baina ya vyombo vya habari na baadhi ya viongozi serikalini.