Siku ya Alhamisi, huduma muhimu zinazotolewa na mashirika ya serikali ikiwa ni pamoja na tuvuti ya e-Citizen, Huduma za ununuzi wa token za KPLC, shirika la reli nchini, NTSA, Mpesa, Benki ya Standard Chartered na benki ya ABSA yaliathirika na jaribio la udukuzi.
Waziri Eliud Owalo alithibitisha shambulio katika huduma za e-Citizen lakini akasema hakuna data iliyoathiriwa.
Huduma katika tuvuti hiyo hata hivyo ziliweza kurejeshwa baada ya wataalam akatika wazara ya ICT kuingililia kati.
Alhamisi jioni, Kampuni ya Kenya Power and Lighting ilisema mfumo wake ulikumbwa na hitilafu ya mtandao na kusababisha kutopatikana kwa baadhi ya huduma ikiwa ni pamoja na ununuzi wa token kutumia USSD na Mpesa.