Wakili PLO Lumumba amemtaka kinara wa Azimio Raila Odinga kuwaeleza Wakenya jinsi kumwalika mgeni kusuluhisha masuala ya nyumbani kutakomesha gharama ya juu ya maisha.
Lumumba amewashutumu viongozi wa Azimio kwa kuwa wanafiki na kukataa kufichua ajenda halisi ya maandamano.
Lumumba ametaka kujua jinsi Rais Ramaphosa au Samia Suluhu watamsaidia Ruto, Raila kupunguza gharama ya maisha.
Amewashutumu viongozi wa Azimio kwa kutumia damu ya wananchi wasio na hatia kutafuta madaraka kupitia mlango wa nyuma.
"Mzee Raila Odinga, Tafadhali waambie Wakenya kwa nini tunahitaji Waafrika wengine wenye nia njema kutatua masuala yetu ya ndani yanayohusiana na Mswada wa Fedha na Gharama ya Maisha wakati tuna Wabunge wanaolipwa sana na Viongozi wengine waliochaguliwa. @WilliamsRuto@RailaOdinga@skmusyoka@EugeneLWamalwa."
Swali la Lumumba limeibuliwa na Wakenya wengi wanaotaka kuelewa kile Raila Odinga anapigania. Watu wamekufa katika maandamano lakini kiongozi anatafuta tu mamlaka ili kuhifadhi maslahi yake binafsi.
Rais Ruto hata hivyo ameweka wazi kuwa, anatafuta kufanya mazungumzo na kinara wa Azimio Raila Odinga kuhusu masuala ya gharama ya juu ya maisha.
Mzee Raila Odinga, Kindly tell Kenyans why we need other Africans of goodwill to solve our domestic issues relating to Finance Bill and Cost of Living when we have highly paid Parliamentarians and other elected Officials. @WilliamsRuto @RailaOdinga @skmusyoka @EugeneLWamalwa pic.twitter.com/5YMVuyE9bW
— PLO Lumumba (@ProfPLOLumumba) July 28, 2023
Rais anawataka wapinzani kutoa suluhu lao la muda mrefu la gharama za maisha na kuacha kucheza ngoma kwenye makaburi ya raia wa kawaida waliofariki katika maandamano.
Matamsho ya wakili huyo yanajiri siku chache baada ya kiongozi wa Azimio kudai Rais wa Tanzania alikuwa Nchini kumpatanisha na ruto.
Huku Ikulu ikijibu madai ya Railan ilisema kwamba Ruto hakumualika Suluhu nchini.
Raila alisema wakati wa mazungumzo na Ruto lazima kuwe na Rais wa nchi ngine au Rais mstaafu, pia alidai kwamba ruto hataki Rais Ramaphosa kuwapatanisha.