Wakili Otiende Amollo amemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi Japheth kuheshimu utakatifu wa ubinadamu.
Ni wazi kwamba, madai ya Koome dhidi ya viongozi wa Azimio-OKA ni ya kutisha na ya kusikitisha mno.
Otiende Amollo amemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi Japheth Koome kuhisi uchungu wa kufiwa na mpendwa wake na akome kutoroka majukumu.
"IG Koome, Acha Kucheza Kwenye Makaburi ya Wale Uliowaua Kikatili!"Amollo aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter.
Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome amedai kuwa upinzani ulikodisha maiti ili kuvutia hisia za kisiasa kutoka kwa Wakenya huku Azimio na serikali wakizozana kuhusu maandamano dhidi ya serikali.
Bila kutoa madhubuti kuunga mkono madai yake, askari huyo mkuu, alipokuwa akiwahutubia wanahabari Jumanne, Agosti 8, alidai kuwa viongozi wakuu wa upinzani ambao hakuwataja majina, walikodisha maiti kutoka vyumba vya kuhifadhia maiti kote nchini kwa nia ya kuwaonyesha kama matokeo ya ukatili wa polisi.
"Watu hawa wanawezaje kuwa viongozi wa jamii? Kama polisi, tuna jukumu la kulinda maisha na mali. Propaganda hazitatuvunja moyo," Koome alidai.
Wakati huo huo, IG Koome pia alitaka Azimio kuhusu mpango wao wa kuwasilisha kesi ya ukatili wa polisi katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) akidai kuwa hatua hiyo inalenga kuwavunja moyo maafisa wa polisi.