Ninasalia ODM hadi Raila awasiliane nami - Jalang'o

Matamshi ya mbunge huyo yalifuatia kauli ya Jumatano ya Baraza Kuu la Kitaifa la chama cha ODM kwamba amefukuzwa

Muhtasari
  • Alisisitiza kwamba atasalia kuwa mwanachama wa Bunge la Kitaifa la Eneo Bunge la Lang'ata, hadi uchaguzi mkuu ujao wa 2027.
  • Kufuatia hatua hiyo, mtangazaji huyo wa zamani wa redio alizamia kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo alishiriki ujumbe wa kujitia moyo.

Mbunfe Jalang'o asema hajutii kuutana na rais
Mbunfe Jalang'o asema hajutii kuutana na rais
Image: Instagram

Mbunge wa Lang'ata Phelix Odiwuor almaarufu Jalang'o sasa anasema kwamba anasalia kuwa mwanachama wa Orange Democratic Movement (ODM) hadi atakapopokea mawasiliano kutoka kwa mmiliki wake.

Akizungumza na Redio 47, Jalang'o alisema hajapokea mawasiliano yoyote kuhusu kufukuzwa kwa kiongozi wa chama Raila Odinga.

Alisisitiza kwamba atasalia kuwa mwanachama wa Bunge la Kitaifa la Eneo Bunge la Lang'ata, hadi uchaguzi mkuu ujao wa 2027.

"Chama ni cha Raila Amollo Odinga na kama sijapata habari kutoka kwa Raila mimi ni mwana ODM... Mbunge wa Lang'ata hadi 2027 ni mimi Phelix Odiwuor Jalang'o. Nataka uchukue hii habari ninakuambia upeleke benki wakukope pesa kwa sababu ndio ukweli. Hakuna mabadiliko," Jalang'o alisema.

Matamshi ya mbunge huyo yalifuatia kauli ya Jumatano ya Baraza Kuu la Kitaifa la chama cha ODM kwamba amefukuzwa uanachama pamoja na wabunge wengine wanne walioasi.

Waliojumuisha Elisha Ochieng’ Odhiambo (Gem), Caroli Omondi (Suba Kusini), Gideon Ochanda (Bondo), na Tom Ojienda (Seneta wa Kaunti ya Kisumu).

Walitimuliwa katika NEC iliyoitishwa na Raila Odinga.

Ilikuja karibu mwezi mmoja baada ya wajumbe walioasi kufika mbele ya kamati inayoongozwa na Sihanya kujitetea kutokana na tuhuma za utovu wa nidhamu uliokithiri.

Kufuatia hatua hiyo, mtangazaji huyo wa zamani wa redio alizamia kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo alishiriki ujumbe wa kujitia moyo.

"Hakuna jaribio ambalo ni nzito sana kuinua!," Jalang'o aliandika.

Mbunge huyo wa muhula wa kwanza aliambatanisha taarifa yake na picha yake ya kumbukumbu ya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana ambapo alionekana akiwa amebeba sanduku kubwa la ushahidi mahakamani wakati wa kesi ya Azimio la Umoja dhidi ya ushindi wa rais William Samoei Ruto.

Kuongeza kwenye kauli yake, Jalang’o pia alishiriki mstari wa Biblia kutoka kwa kitabu cha Wakorintho 10:3 ambao unazungumza kuhusu Mungu kuwasaidia watu Wake kushinda majaribu.

“Hakuna jarabio lililokupita ambalo si kawaida ya kwa wanadamu. Mungu ni mwaminifu, naye hatawaacha mjaribiwe kupita mnavyoweza, bali pamoja na lile jaribio atatengeneza na mlango wa kutokea, ili mweze kulistahimili,” mstari huo wa Biblia unasema.