Ripoti: Idadi ya watu wanaotumia bangi yaongezeka kwa asilimia 90 katika miaka 5

Takwimu mpya zinaonyesha mienendo ya kushangaza katika kuanza na kutumia dawa za kulevya.

Muhtasari
  • Takwimu zilizotolewa na Nacada zilizoainishwa katika ripoti ya kina, zinaelezea zaidi kuhusu uzito wa tatizo hilo.

Utafiti mpya wa mamlaka ya kitaifa ya kupambana na matumizi mabaya ya pombe na madawa ya kulevya (Nacada) unaonyeshakuwa matumizi ya mihadarati nchini humo yameibua wasi wasi mkubwa kuhusu kuennea kwa matumizi ya bangi miongoni mwa vijana wadogo.

Idadi ya watu wanaotumia bangi nchini Kenya ilikaribia kuongezeka maradufu katika miaka 5 - ripoti ya Nacada ilionyesha.

Takwimu mpya zinaonyesha mienendo ya kushangaza katika kuanza na kutumia dawa za kulevya.

Zinaonyesha kuwa umri wa chini wa kuanza kutumia vilevi mbali mbali ikiwa ni pamoja na tumbaku pombe na madawa ya kulevya ni mdogo sana, hadi watoto wenye umri wa miaka sita wameingizwa katika matumizi ya tumbaku.

Imeonekana pia kuwa matumizi ya madawa ya kulevyakama vile heroni, huanza kutumiwa miongoni mwa watoto wenye umri mdogokuanzia miaka minane,na kumi na minne., wakati matumizi ya kokeini huanza katika umri wa miaka ishirini.

Ripoti hiyo inaangazia kuongezakkaribu mara dufu kwa matumizi ya bangi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita na hivyo kuibua wasiwasi kuhusu kuenea taarifa potofu na Imani potofu zinazohusu madhara yake., hususan miongoni mwa vijana.

Takwimu zilizotolewa na Nacada zilizoainishwa katika ripoti ya kina, zinaelezea zaidi kuhusu uzito wa tatizo hilo.

Magharibi mwa Kenya imeongoza katika orodha ya mikoa yenye kuenea zaidi kwa ulevi nchini Kenya, kulingana na uchunguzi uliofanywa na Mamlaka ya Kitaifa ya Kampeni Dhidi ya Matumizi Mabaya ya Pombe na Madawa ya Kulevya (Nacada).

Utafiti huo uliotolewa Jumatatu tarehe 11, ulifichua kuwa eneo la Magharibi lina kiwango cha unywaji pombe cha asilimia 26.4, huku eneo la Pwani likishika nafasi ya pili kwa kiwango cha asilimia 13.9. Kenya ya Kati ilifunga nafasi ya tatu kwa kiwango cha asilimia 12.8.

Linapokuja suala la unywaji wa Chang’aa, pombe asilia inayotengenezwa kutokana na uchachushaji wa nafaka kama mtama, tena, eneo la Magharibi liliongoza kwa kiwango cha asilimia 11.4 ikifuatiwa na Nyanza kwa asilimia 6.3. Eneo la Bonde la Ufa lilishika nafasi ya tatu kwa kiwango cha matumizi cha asilimia 3.6.