•"Maeneo yaliyoorodheshwa yataathiriwa na kukatizwa kwa umeme kesho (12 Septemba, 2023). Kukatizwa huko ni sehemu ya matengenezo ya mtandao,” KPLC ilitangaza.
•Baadhi ya maeneo ya Waiyaki Way eneo la Kangemi, Kaunti ya Nairobi yataathiriwa kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kutakuwa na kukatizwa kwa umeme katika baadhi ya maeneo ya nchi kwa muda mrefu siku ya leo, Jumanne, Septemba 12, KPLC ilitangaza.
Katika taarifa ya Jumatatu jioni, kampuni ya kusambaza umeme ya KPLC ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti nane yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
"Maeneo yaliyoorodheshwa yataathiriwa na kukatizwa kwa umeme kesho (12 Septemba, 2023). Kukatizwa huko ni sehemu ya matengenezo ya mtandao,” KPLC ilitangaza Jumatatu jioni.
Kulingana na taarifa hiyo, baadhi ya maeneo ya Waiyaki Way eneo la Kangemi, Kaunti ya Nairobi yataathiriwa kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya maeneo ya eneo la Njiru na eneo la shule ya Mwangaza ya jiji la Nairobi pia yatakuwa bila umeme kwa muda mwingi wa siku.
Katika Kaunti ya Nakuru, eneo lote la White House na sehemu za Kiti zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na tisa alasiri. Eneo lote la Sobea na Gicheha Farm pia litaathirika kwa wakati mmoja.
Maeneo ya Tola, Bob Harris, TIBS na Witeithie katika Kaunti ya Kiambu pia yataathiriwa na kupotea kwa umeme kati ya 9AM na 5PM jioni.
Katika Kaunti ya Mombasa, sehemu ya eneo la Nyali na Bamburi haitakuwa na nguvu kati ya saa tatu asubuhi na kumi na moja jioni.
Sehemu za kaunti ya Trans Nzoia katika maeneo ya Maili Saba na Sibianga pia hazitakuwa na umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Maeneo ya Nyamarambe na Riosiri katika Kaunti ya Migori pia yataathirika kwa wakati mmoja.
Katika Kaunti ya Meru, Mji wa Maua, eneo la Athi na eneo la Kiegioi hakutakuwa na umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kiumi jioni. Pia litakaloathiriwa wakati huo huo ni eneo la Masinga katika Kaunti ya Embu.