Tazama maeneo ambayo yatakuwa bila stima Jumatano, Septemba 13- KPLC

KPLC imetangaza kuwa maeneo kadhaa katika kaunti 8 za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi jioni.

Muhtasari

•KPLC ilitoa ilani kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa siku ya Jumatano, Septemba 13.

•Kaunti zitakazoathirika ni pamoja na Nyeri, Meru, Embu, Homa Bay, Siaya, Elgeyo Marakwet, Trans Nzoia na Uasin Gishu.

Kenya Power
Image: HISANI

Jumanne jioni, Kampuni ya Kusambaza Umeme Nchini (KPLC)  ilitoa ilani kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa siku ya Jumatano, Septemba 13.

Katika taarifa yake, kampuni hiyo ilitangaza kuwa maeneo kadhaa katika kaunti nane za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi jioni.

Kaunti zitakazoathirika ni pamoja na Nyeri, Meru, Embu, Homa Bay, Siaya, Elgeyo Marakwet, Trans Nzoia na Uasin Gishu.

Katika Kaunti ya Nyeri, maeneo ya Kamacharia na Kamune yataathiriwa na kupotea kwa umeme kutoka saa tatu  asubuhi hadi saa tisa alasiri.

Maeneo ya KWS, Kinna na Prison katika kaunti ya Meru yatakosa umeme kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi jioni.

Maeneo yatakayoathirika katika kaunti ya Embu ni pamoja na Kiritiri na Rugongwe ambayo yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na kumi jioni.

Katika kaunti ya Homa Bay, maeneo ya Marindi, Murram na Ombo yatakosa umeme kati ya tatu asubuhi na tisa alasiri.

Sehemu ya eneo la Chepkongi Primary katika kaunti ya Uasin Gishu itaathirika kati ya saa nne asubuhi na kumi  jioni.

Katika Kaunti ya Trans Nzoia, maeneo ya Mois Bridge na Matunda yataathirika kati ya tatu asubuhi na tisa alasiri wakati eneo la Hospitali ya Siaya katika Kaunti ya Siaya likikosa umeme kati ya saa tatu asubuhi hadi nane alasiri.

Maeneo yatakayoathirika katika kaunti ya Elgeyo Marakwet ni pamoja na Kessup Sawmill na Zahanati ya Kapcherop ambayo itaathirika kati ya tatu asubuhi na tisa alasiri.