Fahamu maeneo ya Kenya ambayo yatakuwa bila stima Alhamisi- KPLC

Kaunti zitakazoathirika ni pamoja na Nairobi, Kiambu, Uasin Gishu, Trans Nzoia, Nyeri, Meru Muranga, Kirinyaga, Mombasa na Kilifi.

Muhtasari

•Maeneo kadhaa katika takriban kaunti kumi za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni.

•Maeneo ambayo yataathirika katika kaunti ya Nairobi ni pamoja na sehemu ya Riverside Drive, Joska, Thomena sehemu ya Mpaka Road

Image: MAKTABA

Kampuni ya Kusambaza Umeme Nchini (KPLC) kwa mara nyingine imetangaza kukatizwa kwa umeme ambako kumepangwa kufanyika siku ya Alhamisi, Septemba 14.

Maeneo kadhaa katika takriban kaunti kumi za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kiambu, Uasin Gishu, Trans Nzoia, Nyeri, Meru Muranga, Kirinyaga, Mombasa na Kilifi.

Maeneo ambayo yataathirika katika kaunti ya Nairobi ni pamoja na sehemu ya Riverside Drive, Joska, Thomena sehemu ya Mpaka Road. Stima katika maeneo hayo zimeratibiwa kutokuwepo kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Kiambu, maeneo ambayo yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni ni pamoja na sehemu za Kabete, Kingeero, Wangige, Karagi Estate, Kahuguini na Corner Brook.

Maeneo ya Motosiet na Kachibora katika kaunti ya Trans Nzoia yatakabiliwa na ukosefu wa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.  

Maeneo la Jabali na Karara Farm katika kaunti ya Uasin Gishu pia yatakosa nguvu za umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi jioni. Katika kaunti ya Nyeri, maeneo ambayo yataathirika ni pamoja na Witima na Kagumo ambako hakutakuwa na stima kati ya saa  tatu asubuhi na saa kumi jioni.

Katika kaunti ya Mombasa, baadhi ya sehemu za eneo la Port Reitz zitakosa stima kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kilifi, sehemu ya eneo la Gotani itaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi jioni.

Maeneo ya Laare na Mutuati katika kaunti ya Meru pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi jioni.