Huzuni!Mwanamume aaga dunia siku ya harusi yake Kangundo

Sherehe hiyo ilipaswa kuwa upya wa viapo pamoja na uthibitisho wa kanisa.

Muhtasari
  • Mary Musyoki alipaswa kufanya upya viapo vyake vya harusi na mumewe, Michael katika Kanisa Katoliki la Kamanzi Kaunti ya Machakos.
crime scene
crime scene

Mwanamke mmoja ambaye alitarajiwa kurejelea viapo vyake  vya ndoa siku ya Jumamosi aliachwa mjane baada ya mume wake kuanduka kwenye bafu alipokuwa akioga kujiandaa kwa ajili ya siku yake ya kipekee..

Mary Musyoki alipaswa kufanya upya viapo vyake vya harusi na mumewe, Michael katika Kanisa Katoliki la Kamanzi Kaunti ya Machakos.

Michael alikimbizwa hospitalini lakini alitangazwa kuwa amefariki alipofika.

Mary akizungumza na vyombo vya habari siku ya JUmamose alisema kuwa;

"Alianguka alipokuwa anaoga kujitayarisha, tulimpeleka hospitali lakini alitangazwa kuga dunia baada ya kufika."

Mwili wake ulipelekwa kwa makafani  ya Kivaani na familia ikarejea nyumbani kujiandaa kwenda kanisani licha ya mkasa huo.

Sherehe hiyo ilipaswa kuwa upya wa viapo pamoja na uthibitisho wa kanisa.

Misa hiyo iliongozwa na Fr Jones Muinde.

Kisha familia ilienda kwa mapokezi katika Shule ya Msingi ya Kamanzi iliyo karibu.