Uwakilishi wa Wafanyakazi ni muhimu katika Bodi ya EPRA - Atwoli

Haya yanajiri siku chache baada ya shirika la mamlaka ya udhibiti wa Nishati na Petroli kuongeza bei za mafuta

Muhtasari

• Muhimu katika wito huu ni kwamba, kuwa na mwakilishi wa COTU (K) katika Bodi ya EPRA kungehakikisha ustawi wa wafanyikazi katika sekta ya kawi.

Francis Atwoli/COTU Secretary General.
FRANCIS ATWOLI Francis Atwoli/COTU Secretary General.
Image: CHARLENE MALWA

Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi (COTU), Francis Atwoli, anahimiza Sheria ya Kawi ya 2019 Kifungu cha 12 kibadilishwe ili kujumuisha uwakilishi wa mashirika ya wafanyikazi katika Bodi ya EPRA, kama ilivyokuwa hapo awali.

Muhimu katika wito huu ni kwamba, kuwa na mwakilishi wa COTU (K) katika Bodi ya EPRA kungehakikisha ustawi wa wafanyikazi katika sekta ya kawi.

Atwoli alisema kuwa;

“COTU (K) inawakilisha maslahi ya wafanyakazi katika sekta mbalimbali, zikiwemo zile za sekta ya kawi. Kwa kuzingatia athari kubwa za bei ya umeme kwa wafanyikazi na kaya zao, wafanyikazi lazima wawakilishwe kwenye Bodi ya EPRA," 

 Alisisitiza kuwa, utaalamu wa COTU katika sekta ya nishati, ni ujuzi wao wa masuala ya kazi na utata wa soko la nishati unaweza  kuimarisha mijadala ndani ya Bodi ya EPRA, na hivyo kusababisha maamuzi sahihi zaidi.

Katibu huyo ameeleza kwa kusisitiza kuwa  wawakilishi wa wafanyakazi wanaweza kutumika kama daraja kati ya wafanya kazi na EPRA

"COTU (K) itafanya kazi kama kiunganishi kati ya wafanyikazi na EPRA, kukuza mawasiliano bora na uelewa wa mitazamo ya kila mmoja,Kujumuishwa kwa wawakilishi wa COTU (K) katika michakato ya kufanya maamuzi kutakuza ushirikiano na mazungumzo yenye kujenga."

Mwenyekiti alitaka mapitio ya kina ya Kifungu cha 12 cha Sheria ya Nishati, 2019, ili kuwezesha uwakilishi wa wafanyakazi kwenye Bodi ya EPRA.

Alidai kuwa marekebisho hayo yatasababisha mkabala wa usawa na ujumuishi zaidi wa maamuzi ya bei ya nishati ambayo yatanufaisha wafanyakazi na watumiaji.

"Kujumuishwa kwa wahusika mbalimbali wakuu kama COTU (K) katika bodi ya EPRA kunaongeza uwazi katika maamuzi ya udhibiti. Inahakikisha kwamba maslahi ya makundi mbalimbali ya jamii yanazingatiwa, na hivyo kukuza imani kubwa ya umma katika mchakato wa udhibiti, "

Atwoli amewataka watunga sera kutii wito huu na kuzingatia athari pana za kujumuisha wafanyikazi katika kuunda mazingira ya nishati nchini Kenya.