Kampuni ya Kusambaza Umeme Nchini (KPLC) kwa mara nyingine imetangaza kukatizwa kwa umeme ambako kumepangwa kufanyika siku ya Alhamisi, Septemba 28.
Maeneo kadhaa katika takriban kaunti tisa za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kiambu, Uasin Gishu, Kisumu, Kilifi, Trans Nzoia, West Pokot, Migori, Embu na Isiolo.
Katika kaunti ya Nairobi, maeneo ambayo yatakosa stima kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni ni pamoja na Muthaiga, Saika, Umoja, sehenu ya Kangundo Road, Uwanja wa ndege wa Wilson na sehemu ya Lang'ata Road.
Maeneo ya Kokotoni na Jimba katika kaunti ya Kilifi pia yataathika na ukosefu wa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Katika kaunti ya Kisumu, sehemu ya eneo la Ujenzi Quarry itakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.
Wakati uo huo, maeneo ya Karamu na Mabera katika kaunti ya Migori yataathiriwa na kukatizwa kwa nguvu za umeme.
Maeneo ya Red Hill Villas, Kigwa Farm na Fourways katika kaunti ya Kiambu yatashuhudia kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni siku ya Alhamisi.
Mji mzima wa Isiolo katika kaunti ya Isiolo utakosa huduma za umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Katika kaunti ya Embu, maeneo ya Gatondo na Muchonoke yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Aidha, sehemu za maeneo ya Kapenguria na Maili Saba katika kaunti za Trans Nzoia na West Pokot yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.