Polisi huko Elgeyo Marakwet wanachunguza kisa ambapo mwanamke mmoja aliwakatakata watu watatu hadi kufa, akiwemo mtoto wake wa miezi mitatu.
Kulingana na walioshuhudia, mwanamke huyo alizinduka Jumapili usiku, akaokota panga, na kuwashukia watu watatu eneo la Elgeyo Marakwet eneo la Katilit.
Watu wawili zaidi walijeruhiwa wakati wa shambulio hilo la usiku na kupelekwa katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi, ambapo wamelazwa kwa matibabu.
Bado haijabainika sababu ya mauaji hayo, lakini polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu suala hilo.
Haya yanajiri miezi michache baada ya mwanamke mmoja Kitebngela kumkatakata na kumla mwanawe, baada ya kukosana na baba ya mtoto wake.