Kenya kuondoa nyumba za watoto za kibinafsi, Serikali ya Kenya imetangaza kufunga nyumba zote za watoto zinazomilikiwa na watu binafsi ndani ya miaka minane, ikisema hilo litasaidia kwa kiasi kukomesha ulanguzi wa watoto.
"Katika miaka minane ijayo nyumba za kibinafsi hazitakuwepo."
Tunahitaji kujiandaa ili kuwaweka katika mazingira mazuri watoto hao ambao watatoka katika nyumba za kibinafsi," Waziri wa Kazi na maendeleo ya Jamii Florence Bore alisema katika hafla siku ya Jumapili.
Bi Bore alikuwa amechapisha kwenye X (zamani Twitter) mapema Jumamosi kwamba serikali tayari ilikuwa katika harakati za kufunga nyumba za watoto na yatima.
Alisema watoto katika taasisi hizo watawekwa katika malezi ya familia na jamii, jambo ambalo alisema linatoa mazingira bora kwa watoto hao. Wenyeji wanasema kuna zaidi ya watoto 40,000 katika takriban nyumba 800 za kulea nchini Kenya.
Mengi ya haya yanafikiriwa kuendeshwa kibinafsi.
Kenya imekuwa ikitafuta kuondoa nyumba za kibinafsi za watoto na nyumba za watoto yatima tangu kupitishwa kwa Sheria ya Mtoto ya 2022, ambayo inataka mabadiliko ya ulezi, uwekaji wa malezi na kuasili.