Serikali inapanga kufuta ushuru wa gesi ya kupikia baada ya bei kupanda kwa Sh 260

Pendekezo hilo linakuja siku chache baada ya bei ya reja reja ya gesi ya kupikia kupanda kwa angalau Sh260 kwa mtungi wa kilo 13 hadi Sh3,160 kutoka Sh2,900 mwezi Julai.

Muhtasari

• Sheria ya Fedha ya 2023 iliyoanza kutumika kuanzia Julai iliondoa gesi ya kupikia kutoka kwa VAT ya asilimia 8.0, IDF ya asilimia 3.5 na asilimia 2.0 ya RDL.

Washukiwa 4 wafikishwa mahakamani kwa kujaza tena gesi za LPG kinyume cha sheria
Image: DCI

Serikali imefichua mpango mpya wa kufuta ushuru wote wa gesi ya kupikia na mitungi huku kukiwa na uwekezaji wa mabilioni ya shilingi katika sekta hiyo katika juhudi za hivi punde za kuharakisha mpito wa Kenya kwa nishati safi, gazeti la Business Daily limeripoti.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, katika kikao cha baraza la mawaziri mapema JUmanne, kupanda tena kwa bei ya gesi ya kupikia lilikuwa moja ya suala ambalo lilijadiliwa na suluhu kutajwa kuwa ni kufutwa kwa ushuru wote kwa bidhaa hizo.

“Yafuatayo yamependekezwa; kuondolewa kwa ushuru wa mitungi inayotengenezwa nchini, kwenye bidhaa ya gesi ya kimiminika (LPG) pamoja na gharama ya urekebishaji wa silinda,” ilisema ujumbe wa Baraza la Mawaziri jana jioni.

Ushuru pekee unaotozwa kwa LPG ni Ushuru wa Mfuko wa Maendeleo ya Petroli kwa kiwango cha Sh0.40 kwa kilo huku mitungi ya LPG ikivutia ushuru sita, ikijumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa kiwango cha asilimia 8.0, Ada ya Tamko la Uagizaji wa asilimia 3.5 na Ushuru wa Maendeleo ya Reli (RDL) kwa kiwango cha asilimia 2.0 ya thamani ya gharama, bima na mizigo (CIF).

Pendekezo hilo linakuja siku chache baada ya bei ya reja reja ya gesi ya kupikia kupanda kwa angalau Sh260 kwa mtungi wa kilo 13 hadi Sh3,160 kutoka Sh2,900 mwezi Julai.

Gharama ya mtungi huo wa kilo sita pia imepanda hadi Sh1,380 kutoka Sh1,200 katika vituo vya jiji.

Sekta hii imevutia wawekezaji wengi zaidi, ambapo ya hivi punde zaidi ni ile ya Gesi ya Taifa, inayomilikiwa na tajiri wa Kitanzania Rostam Aziz.

Uondoaji wa ushuru huo ulianza katika enzi ya Mwai Kibaki wakati LPG haikuwa na ushuru, na hivyo kusaidia kuweka bei katika wastani wa Sh1,600 kwa kontena la kilo 13 mnamo 2007.

Sheria ya Fedha ya 2023 iliyoanza kutumika kuanzia Julai iliondoa gesi ya kupikia kutoka kwa VAT ya asilimia 8.0, IDF ya asilimia 3.5 na asilimia 2.0 ya RDL.

Bei ya gesi ya kupikia ilikuwa imeshuka kwa Sh430 kwa kontena la kilo 13 na Sh150 kwa silinda ya kilo sita mnamo Julai kufuatia kupunguzwa kwa ushuru.