Waathiriwa wa ubomoaji walipuuza onyo letu - Portland Cement yasema

Aidha wameongeza kuwa kufurushwa kumetekelezwa kwa namna ambayo serikali iliona ni muhimu kufanya.

Muhtasari
  • Mbithi alisema waliendesha kampeni kwenye vyombo vya habari na hata kuwashirikisha wananchi wa eneo hilo wakiwaonya dhidi ya ununuzi wa ardhi hiyo.
Image: ENOS TECHE

Kampuni ya East African Portland Cement plc sasa inasema iliwaonya waathiriwa wa ubomoaji unaoendelea dhidi ya kununua ardhi waliyokaa.

Katika kikao na wanahabari siku ya Jumanne, Mwenyekiti wa Portland Richard Mbithi alisema walitoa maonyo mengi wakisema kwamba ardhi hiyo haiuzwi kwa vile ni mali ya EAPC.

Mbithi alisema waliendesha kampeni kwenye vyombo vya habari na hata kuwashirikisha wananchi wa eneo hilo wakiwaonya dhidi ya ununuzi wa ardhi hiyo.

“Mtu yeyote anayedai umiliki wa ardhi hiyo anachukuliwa kuwa ni maskwota kinyume cha sheria, tuliomba kuwafukuza wanaomiliki ardhi hiyo kinyume cha sheria,” walisema.

Aidha wameongeza kuwa kufurushwa kumetekelezwa kwa namna ambayo serikali iliona ni muhimu kufanya.

"Mahakama haikuzungumzia ubomoaji waliotoa uamuzi huo. Ardhi hiyo haikusudii kuuzwa bali ni matumizi ya serikali," walisema.

Kwa upande wa mazungumzo, MD Oliver Kirubai alisema:

"Viongozi wanaopinga ubomoaji hawajatufikia. Wakishafanya hivyo tutajua njia ya kuendelea," MD alisema.

Kuhusu ardhi iliyopo walisema lango liko wazi kwa maskwota tu kwani watapewa kipaumbele cha kwanza.