logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mvulana 17 amuuwa mwenzake 15 baada ya kuzozania kipande cha muwa – Nakuru

Polisi wako mbioni kuchunguza maafa yaliyosababishwa na  mzozo wa miwa na umbwa

image
na

Makala19 October 2023 - 06:58

Muhtasari


•Kikosi cha wapelelezi kilitembelea eneo la tukio siku ya Jumatano na kupata panga lililotumika katika shambulio la mvulana huyo aliyefariki,Mshambuliaji huyo aliripotiwa kutororoka  na juhudi za kumtafuta zinaendelea

Crime scene

Polisi wanachunguza kifo cha mvulana ambaye alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye vita vya kung'ang'ania kipande cha miwa eneo la Kuresoi, Kaunti ya Nakuru.

Mvulana huyo mwenye umri wa miaka 15 alifariki hospitalini kufuatia jeraha alilopata kichwani baada ya kukatwa na panga  kijana  mwenzake wa miaka 17.

Walioshuhudia kisa hicho walisema kuwa wawili hao walizozana kuhusu kipande cha miwa kabla ya kijana  huyo wa miaka 17 kumkata na kutoroka.

Alikimbizwa hospitalini ambapo alifariki siku ya Jumatano, polisi walisema.

Kikosi cha wapelelezi kilitembelea eneo la tukio siku ya Jumatano na kupata silaha iliyoyumika katika mauaji. Mshukiwa mkuu ameenda mafichoni na anasakwa na polisi.

Polisi walisema mwili wa marehemu ulihamishwa hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.

 Kwingineko Polisi wanamsaka mwanamume aliyemuua mwenzake kwenye mabishano kuhusu mbwa aliyejeruhiwa katika eneo la Mau Summit, Kaunti ya Nakuru.

Kennedy Too alifariki hospitalini baada ya kugongwa kichwani. Hii ni baada ya kumpiga teke mbwa aliyekuwa akivuka barabara karibu na alipokuwa.

Mmiliki wa mbwa huyo Wesley Bett, 27, alikasirishwa na kumpiga kwenye paji la uso kwa kutumia fimbo na kuanguka. 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved