Pasipoti 16,821 ziko tayari kuchukuliwa kuanzia Oktoba 23

Pasipoti zitakusanywa kutoka kwa ofisi za uhamiaji za kanda.

Muhtasari

•Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki ameongeza juhudi za kukomeza ufisadi katika Idara ya Uhamiaji kufuatia kilio cha umma kuhusu kucheleweshwa kwa utayarishaji wa hati za kusafiria

•Jijini Nairobi, pasipoti 7,500 zitakuwa tayari kuchukuliwa Nyayo House, 1,725 Eldoret, 1, 771 Embu, na 1,501 Kisii

Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki akiwa Nyayo House Jumanne, Novemba 29. Picha: MINA
Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki akiwa Nyayo House Jumanne, Novemba 29. Picha: MINA

Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki ameongeza juhudi za kukomesha ufisadi katika idara ya Uhamiaji kufuatia kilio cha umma kuhusu kucheleweshwa kwa utayarishaji wa hati za kusafiria.

Uwasilishaji wa pasipoti za kitaifa utaendelea hadi wiki ya tatu, huku pasi 16,821 zikiwa tayari kuchukuliwa kuanzia Jumatatu.

Wizara ya Mambo ya Ndani imetangaza kuwa pasi hizo zitachukuliwa kutoka kwa ofisi za Uhamiaji za  kanda kuanzia Oktoba 23 hadi Ijumaa, Oktoba 27, 2023.

Jijini Nairobi, pasi 7,500 zitakuwa tayari kuchukuliwa Nyayo House, 1,725 Eldoret, 1, 771 Embu, na 1,501 Kisii.

Mjini Nakuru, pasipoti 1,002 ziko tayari huku 1,547 zikiwa zimechapishwa na kusubiri kukusanywa Mombasa. Mjini Kisumu, idara hiyo ilisema pasi 1,262 ziko tayari kuchukuliwa wiki ijayo.

Baadhi ya pasi 15, 354 zilitumwa katika wiki ya pili ya Oktoba 2 na 6. Wiki hii, pasipoti 13, 290 kwa sasa zinakusanywa kutoka Jumatatu, Oktoba 16, hadi Alhamisi, Oktoba 19.

Serikali ilionya kuwa hati za kusafiria ambazo hazijachukuliwa baada ya muda uliopangwa kuchukuliwa zitatupwa na wamiliki kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria.