logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Majambazi wampora bosi wa polisi bastola yake Kiambu

Polisi wameanzisha msako kuwakamata wahalifu hao na kupata bunduki hiyo.

image
na Radio Jambo

Habari23 October 2023 - 12:34

Muhtasari


  • Kulingana na ripoti za polisi, inspekta huyo alivamiwa na genge la watu watatu ambao pia walikuwa na silaha na kutoroka na bastola yake na karibu risasi 15.

Inspekta wa polisi alivamiwa na kuporwa bastola Jumatatu katika eneo la Kingeero, Kaunti ya Kiambu.

Inspekta huyo ambaye jina lake halikutajwa mara moja, anasimamia Kituo cha Polisi cha Mwimuto kaunti ya Kiambu.

Kulingana na ripoti za polisi, inspekta huyo alivamiwa na genge la watu watatu ambao pia walikuwa na silaha na kutoroka na bastola yake na karibu risasi 15.

Afisa huyo alivamiwa kwenye lango la mwenzake alipoenda kuzungumzia uchunguzi unaoendelea wakati kisa hicho kilipotokea.

Akiwa anasubiri kufunguliwa geti, waliibuka watatu hao wakiwa wamechukua bunduki yake ya utumishi na risasi.

Pia waliiba pesa taslimu na simu ambayo afisa huyo alikuwa nayo, kabla ya kutoweka gizani.

Kisa hicho kilitokea mwendo wa saa moja asubuhi Jumatatu, kulingana na rekodi za polisi.

Polisi wameanzisha msako kuwakamata wahalifu hao na kupata bunduki hiyo.

Viwango vya uhalifu vimepanda nchini na nyakati ngumu za kiuchumi na kuongezeka kwa ukosefu wa ajira kunawafanya vijana kukata tamaa.

Visa vya wizi na watu kuchomwa visu katika maeneo makubwa ya mijini vimeongezeka huku baadhi ya Wakenya wakilaumu vyombo vya usalama kwa ulegevu.

Siku ya Jumamosi, mtu aliyejihami kwa bunduki anayeshukiwa kuwa mgeni aliwashambulia walinzi wa Mshauri wa Usalama wa Kitaifa Monica Juma, na kusababisha kifo chake baada ya maafisa waliotolewa kutoka kwa polisi wa kijeshi kufyatua risasi.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved