•Mamlaka hii ni shirika la serikali linalomilikiwa kikamilifu lililoanzishwa kupitia Sheria ya Bunge mnamo Januari 1978 likifanya kazi chini ya Wizara ya Barabara na Uchukuzi
Mamlaka ya Bandari ya Kenya imetangaza nafasi 150 za mafunzo ya kazi katika shirika hilo.
Mamlaka hii ya KPA ilisema haswa kuwa kuna nafasi 10 za waendeshaji wa vituo vya kontena na 14 kwa waendeshaji mizigo ya kawaida.
Zaidi ya hayo, nafasi sita zinapatikana katika Teknolojia ya Mawasiliano ya Habari, Uvumbuzi, na Uhandisi upya wa Biashara
Pia kuna fursa tisa kwa Waendeshaji wa Feri na Wahudumu wa Feri.
"Waombaji wanaovutiwa na fursa hizi wanashauriwa kutuma maombi yao mtandaoni pekee kupitia tovuti ya kazi ya Mamlaka ya Bandari ya Kenya.
https://forms.office.com/r/PY22Dy13Hf," KPA ilisema.
"Ili kuhitimu, mwombaji lazima awe Raia wa Kenya asiyezidi miaka 34, awe mhitimu asiye na ajira kutoka taasisi ya mafunzo inayotambulika ambaye amemaliza kozi ya shahada / diploma / na hajapata uzoefu wowote wa kazi kuhusiana na eneo lao,"KPA ilisema.
KPA ilisisitiza kwamba ni lazima maombi yote yapokelewe kabla ya tarehe 27 Novemba 2023.
Mamlaka ni shirika la serikali linalomilikiwa kikamilifu lililoanzishwa kupitia Sheria ya Bunge mnamo Januari 1978 likifanya kazi chini ya Wizara ya Barabara na Uchukuzi.
KPA imepewa mamlaka ya kusimamia na kuendesha bandari zote zilizoratibiwa na bandari za njia ya maji nchini Kenya.