Kiambu: Mwanamume apigwa na umeme hadi kufa akijaribu kumuibia bosi wake kahawa

Baada ya uchunguzi wa kina, walibaini kwamba jamaa huyo alikwenda kwa lengo la kuiba kahawa za mwajiri wake.

Muhtasari

• Baada ya uchunguzi wa kina, walibaini kwamba jamaa huyo alikwenda kwa lengo la kuiba kahawa za mwajiri wake.

Mtambo wa nyaya za stima
Mtambo wa nyaya za stima
Image: Screenshot

Mwanamume mmoja amefariki kwa kupigwa na umeme akiwa katika mchakato wa kuvizia kahawa na bosi wake kwa lengo la kuiiba.

Kwa mujibu wa Nation, jamaa huyo wa umri wa makamo alitambulika kama Evans Njoroge alipatikana amekauka katika mtaro ambako alikuwa anavizia kahawa hiyo ambayo ilikuwa imewekwa ili kukauka.

Polisi walipofika kwenye eneo la tukio, walimpata marehemu na kand yake nusu gunia ya kahawa hizo ambazo anashukiwa alikuwa katika harakati za kuiba.

Baada ya uchunguzi wa kina, walibaini kwamba jamaa huyo alikwenda kwa lengo la kuiba kahawa za mwajiri wake.

“Wakati alipokuwa anaondoka katika kiwanda, aligusa nyaya ya umeme ambayo imetumika kama ua la kuzunguka kiwanda hicho na hapo ndipo alianguka kwenye mtaro,” repoti ya polisi ilisoma.

Mwili wake uliondolewa sehemu hiyo na kusafirishwa hadi makafani ya Kigumo kwa uchunguzi Zaidi.