[PICHA] NTSA yaadhimisha Siku ya Kumbukumbu kwa waathiriwa wa ajali za barabarani

NTSA na wadau wengine walifanya maandamano kuelekea Delamare Naivasha kuwakumbuka waliopoteza maisha au kujeruhiwa kupitia ajali za barabarani.

Muhtasari

•Umoja wa Mataifa mwaka 2005 uliidhinisha kuwa  siku ya kimataifa ya kuadhimishwa kila Jumapili ya tatu mwezi Novemba.

• Idadi ya waliopoteza maisha katika ajali za barabarani mnamo 2021 ilikuwa 4,579.

Image: NTSA

Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama (NTSA) Jumapili iliadhimisha Siku ya Dunia ya Kuwakumbuka waathiriwa wa ajali za barabarani.

NTSA na wadau wengine walifanya maandamano kuelekea Delamare Naivasha kuwakumbuka waliopoteza maisha au kujeruhiwa kupitia ajali za barabarani.

Image: WILLIAM ADUR//THE STAR

Umoja wa Mataifa mwaka 2005 uliidhinisha kuwa siku ya kimataifa ya kuadhimishwa kila Jumapili ya tatu mwezi Novemba kila mwaka, kama 'ukumbusho unaofaa kwa waathirika wa majeraha ya barabarani na familia zao'.

Kulingana na UN, lengo la siku hiyo ni kutoa jukwaa kwa wahasiriwa wa trafiki na familia zao kukumbuka watu wote waliouawa na kujeruhiwa vibaya barabarani.

Image: NTSA

Pia inalenga kutambua kazi muhimu ya huduma za dharura na kutetea usaidizi bora kwa waathiriwa wa trafiki barabarani na familia za wahasiriwa.

Utafiti wa Afya ya Idadi ya Watu nchini Kenya wa 2023 unaonyesha kuwa takriban watu 4,690 walipoteza maisha katika barabara za Kenya mwaka wa 2022.

Image: WILLIAM ADUR//THE STAR

Mwaka huo ulirekodi vifo vya ajali za barabarani 21,757, ikiwa ni ongezeko la asilimia 5.5 kutoka vifo 20,625 vilivyoripotiwa mwaka 2021.

Image: NTSA

Idadi ya waliopoteza maisha katika ajali za barabarani mnamo 2021 ilikuwa 4,579.

Image: NTSA

Idadi ya wahasiriwa ambao walipata majeraha mabaya mnamo 2022 ilikuwa 9,935, pungufu kutoka 10,050 ambao walijeruhiwa vibaya mnamo 2021.