Mchungaji Ng’ang’a atoa Sh410k kwa wachuuzi na ushauri wa biashara

Ng`ang`a pia aliwahimiza wafanyabiashara wadogo kuunda kikundi na kusaidiana ili kupanua biashara zao.

Muhtasari

• Katika ibada  mhubiri huyo alitangaza kuwa atawapa wachuuzi hao pesa ambazo zitawasaidia kukuza biashara yao.

• “Ntawapatia kila mtu Sh10,000, nataka muwe na kikundi nyote mjuane muanzishe biashara yenu, muwe na chama yenu,”

Apostle James Ng`ang`a wa kanisa nla Neno Evangelism
Apostle James Ng`ang`a wa kanisa nla Neno Evangelism
Image: HISANI

Mhubiri wa Neno Evangelism, James Ng’ang’a, aliwashangaza  baadhi ya waumini wake  ambao ni wachuuzi kwa jinsi alivyowapiga jeki.

Katika ibada  mhubiri huyo alitangaza kuwa atawapa wachuuzi hao pesa ambazo zitawasaidia kukuza biashara yao.

Ng`ang`a pia aliwahimiza wafanyabiashara wadogo kuunda kikundi na kusaidiana ili kupanua biashara zao.

“Nitawapatia kila mtu Shilingi 10,000, nataka muwe na kikundi nyote mjuane muanzishe biashara yenu, muwe na chama yenu,” Ng’ang’a alisema.

Jambo hili hata hivyo  lilipelekea sifa na ukosoaji kutoka kwa watumiaji wa mtandao. Wengine walidai kuwa hatua hiyo haikuwa ya maana, wakisema kwamba alikuwa amechukua zaidi kutoka kwa waumini kwa njia ya matoleo na zaka, huku wengine wakimpongeza kwa ukarimu wake.

Mhubiri huyu amekuwa akigonga vichwa vya habari mtandaoni kwa sababu mbalimbali. Mnamo Oktoba, aliwaonya wahitimu wa digrii kukaa mbali na kanisa lake, na kuwashauri kuhudhuria makanisa ambayo ibada ni fupi, akimaanisha kuwa kusimamia mambo ya kiroho kunahitaji mbinu tofauti na ile ya wasomi.

“Wale watu wa digrii, usije kwenye kanisa langu, kwenda kanisa zenu mkaongee dakika mbili mtoke. Na mnakunywa dawa za pressure. Huwezi kudhibiti mambo ya kiroho,” Ng’ang’a alisema.

Mchungaji alisisitiza umuhimu wa kuheshimiana kati ya watu, bila kujali malezi yao ya kielimu.

"Na wale watu wasomi, tafadhali tuheshimiane..." alisema.

Mchungaji Ng’ang’a alichukuwa fursa hiyo kuelezea mtazamo wake kuhusu jinsi watu waliosoma wameathiri vibaya ulimwengu, akiangazia masuala kama vile ushoga.

Alidai kuwa watu wenye elimu wamechangia katika kueneza mambo hayo.

“Wale watu wameharibu dunia nzima ni wasomi. Mimi nilitoka na hii injili 1989. Na nikihubiri nyinyi mnaotaka kuniambia sitahubiri mlikuwa shule mkisomea hizo makaratasi. Na usifikiri mimi utanitisha. Muweke mipaka sababu kuna waganga na wachawi na mnajua mahali wako… Kuna devil worshipers Nairobi, na mnajua,” alisema.

Alitangaza kwamba wale ambao hawatoi matoleo baada ya kupokea upako hawatakaribishwa tena katika kanisa lake.

Mchungaji alisisitiza umuhimu wa michango ya kifedha kutoka kwa waumini, akisisitiza umuhimu wao kwa riziki na uendeshaji wa kanisa.