Waziri wa afya Susan Nakhumincha ampa binti wa rais Charlene Ruto kazi wizarani

"Barua hii ni ya kukuteua kama Balozi wa Damu ya Kenya na kukuomba uendelee kuwa msemaji wa marafiki zako, familia ya vijana wa Kenya, wenzako, na raia wa Kenya" barua ya CS ilisoma.

Muhtasari

• Akionesha shukrani zake kwa kuteuliwa, Binti Ruto alimshukuru waziri Nakhumincha na kusema kwamba amekubali kitengo hicho kipya kwa mikono miwili.

Binti Ruto
Binti Ruto
Image: facebook

Binti wa kwanza wa taifa, Charlene Ruto ameteuliwa kama balozi wa hamasisho la kuchangia damu katika wizara ya afya na waziri Susan Nakhumincha.

 Katika barua ambayo waziri huyo alimuandikia Charlene na ambayo binti Ruto ameipokea kwa mikono wazi na kuipakia kwenye kurasa zake mitandaoni, aliteuliwa kuongoza hamasisho la kuchangia damu kutokana na harakati zake za hivi karibuni kuhusu suala la damu.

"Hii ni kupitia uchangiaji wako wa damu mara kwa mara, utetezi, elimu na uhamasishaji, wanafamilia wako, jamii, wenzako na umma kwa ujumla kushiriki katika uchangiaji wa damu," inasomeka sehemu ya barua hiyo.

Barua hiyo iliyonakiliwa kwa Katibu Mkuu wa Idara ya Serikali ya Huduma za Matibabu inasema zaidi kwamba Wizara ya Afya inatambua jitihada za Charlene za kukusanya rasilimali zinazosaidia shughuli za uchangiaji wa damu na uanzishwaji wa damu.

"Barua hii ni ya kukuteua kama Balozi wa Damu ya Kenya na kukuomba uendelee kuwa msemaji wa marafiki zako, familia ya vijana wa Kenya, wenzako, na raia wa Kenya na kuwashirikisha na kuwahimiza vijana kutoa damu ili kuokoa maisha ya mara kwa mara. muda.," Nakhumicha alisema.

Akionesha shukrani zake kwa kuteuliwa, Binti Ruto alimshukuru waziri Nakhumincha na kusema kwamba amekubali kitengo hicho kipya kwa mikono miwili.

“Asante kwa Wizara ya Afya na Waziri wetu Susan Nakhumicha kwa kunijumuisha katika mpango huu unaoendeshwa na @official_ktta na kuungwa mkono na @kenyan_by_damu. Hebu tuchangie damu!” Charlene alisema.