Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme Jumanne

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Februari 6.

Muhtasari

•KPLC ilisema baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Machakos, Kajiado, Makueni, Uasin Gishu, Kilifi na Mombasa.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Februari 6.

Katika taarifa ya siku ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Machakos, Kajiado, Makueni, Uasin Gishu, Kilifi na Mombasa.

Baadhi ya sehemu za barabara ya Outering na eneo la Donholm Phase 8 katika kaunti ya Nairobi zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Machakos, sehemu kadhaa za maeneo ya Matuu, Sofia, Kyumbi, na Kitui Road  zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tisa asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huo huo, baadhi ya sehemu za maeneo ya Emali Ukia Roa na Kaumoni katika kaunti ya Makueni pia zitakosa umeme.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Kajiado, Kisaju na Isinya katika kaunti ya Kajiado zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Uasin Gishu, sehemu za maeneo ya Burnt Forest na Kondoo zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Kasufini na Mkoamoto katika kaunti ya Uasin Gishu zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tisa asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za eneo la Utange katika kaunti ya Mombasa zitakosa umeme kati ya saa tatu na saa kumi na moja jioni.