Tazama maeneo ya Kenya ambako stima zitapotea Jumatano

KPLC)imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Februari 7.

Muhtasari

•KPLC imetangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti  kumi za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•Baadhi ya sehemu za maeneo ya Huruma, Mbagathi Road na Komarock katika kaunti ya Nairobi zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kenya Power

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Februari 7.

Katika taarifa ya siku ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti  kumi za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Machakos, Kajiado, Nakuru, Siaya, Vihiga, Kisumu, Nyeri, Kirinyaga, na Kiambu.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Huruma, Mbagathi Road na Komarock katika kaunti ya Nairobi zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Machakos, sehemu kadhaa za barabara ya Mombasa zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Kajiado, baadhi ya sehemu za barabara ya Pipeline zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za eneo la Kampi ya Moto katika kaunti ya Nakuru pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Katika kaunti ya Siaya, baadhi ya sehemu za maeneo ya soko la Boro na Hawinga zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa nane mchana.

Soko la Cheptulu katika kaunti ya Vihiga itaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni jioni.

Soko la Chiga katika kaunti ya Kisumu pia itakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri siku ya Jumatano.

Katika kaunti ya Kirinyaga, sehemu kadhaa za maeneo ya Makutano na Sagana zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili unusu na saa saba unusu mchana.

Katika kaunti ya Nyeri, baadhi ya sehemu za maeneo ya Mweiga na Endarasha yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Membley na Kiwania katika eneo la Kaskazini Mashariki zitakosa umeme kati ya saa mbili unusu na saa kumi na moja jioni.